Hadithi za Hekaya - Mhariri Forum

Hadithi ya simba na sungura - sehemu ya 2
Kuna siku Sungura na Simba walibishana kujua nani ana nguvu. Sungura akasema "Mimi nina nguvu." Simba Akajibu "Mimi Ndiyo mwenye nguvu." Sungura akashauri...
"Twende msituni, chukua kamba na tuanze kuvutana kuona nani mwenye nguvu."

Walianza kuvutana kwa kutumia kamba. Simba Alitumia nguvu zake zote mwisho wa siku akachemsha. Kwanini? Sungura mdogo anishinde? Simba akakasirika akenda kuita wenzake, wakaja wakachemsha. Kivipi? Hapa kuna namna. Wale Simba wakaamua kuifuatilia ile kamba, wakagundua Sungura alifunga ile kamba kwenye mti mkubwa.

Hadithi ya simba na sungura - sehemu ya 1
Simba mwenye njaa, katika pitapita zake za kuwinda, alimkuta Sungura akiwa amelala fofofo. Alishusha pumzi, akatabasamu na kumshukuru sana Mungu kwa ukarimu wake wa kutambua taabiko lake na kumtunuku chakula pasi na haja ya kukitolea jasho.

Taratibu alimsogelea Sungura ili asije akamwamsha, akalala yeye…

Alipoinua miguu yake kutaka kumkamata, mara akatokea Ayala mnono ambaye alipita akikimbia karibu naye, akielekea upande wa kaskazini kwenye uwanda wa nyasi fupi.

Simba alimwacha Sungura na akakurupuka kumkimbiza yule Ayala.

Vishindo kelele na purukushani za Simba na Ayala vilimgutusha na kumwamsha Sungura ambaye aliamka na kutimua mbio kuelekea upande wa kusini.

Baada ya kumkimbiza Ayala kwa muda mrefu Simba alishindwa na kuamua kurudi ili akamle yule Sungura.

Alipogundua kuwa Sungura naye alikuwa ameamka na kukimbia, Simba alisema kwa kujilaumu, “ama kweli nimepata nilichostahili; kwa kuwa nilikiacha chakula nilichokitia mkononi tayari kwa tamaa ya kutaka kupata zaidi.”

Hadithi ya Sungura na Fisi: Muhtasari
Zamani za kale, sungura na fisi walipokea barua ya mwaliko wa harusi. Walihitajika kuhudhuria tukio hilo. Sungura aliandaa karanga na kuziweka kwenye mkoba wake, huku fisi akiandaa miogo yake na kuziweka kwenye mkoba wake. Walianza safari yao.

Njiani, sungura alimshawishi fisi kula chakula chake. Sungura alikula chakula cha fisi kidogo kidogo hadi kikamalizika. Waliendelea na safari, wakahisi njaa tena. Fisi alimwomba sungura ampe karanga zake, lakini sungura alikataa akisema karanga zake zina dawa.

Waliendelea na safari, na sungura akapendekeza wabadilishe majina. Sungura alisema ataitwa "Cha Wageni", na fisi ataitwa "Cha Wote". Walipofika, wenyeji waliwakaribisha vizuri na kuwapa chakula, wakisema ni cha wageni. Sungura alikula chakula peke yake.

Asubuhi iliyofuata, wenyeji walileta chakula tena, wakisema ni cha wageni. Fisi alisema hata kama ni cha wageni, yeye atakula. Sungura alimpiga fisi kwa mwiko, na fisi akamrudisha kwa kigoda.