Nyumba za William Ruto

Posted by:

|

On:

|

,

William Ruto ni mwanasiasa wa Kenya ambaye tangu 13 Septemba 2022 amekuwa akihudumu kama rais wa tano wa Kenya. Kabla ya kuwa rais, alihudumu kama naibu wa rais wa kwanza wa Kenya kuchaguliwa, kutoka 2013 hadi 2022.

Hizi hapa ni nyumba ambazo William Ruto anamiliki.

Nyumba za William Ruto

Nyumba ya karen akiwa naibu raisi

Nyumba rasmi ya familia ya William Ruto akiwa naibu raisi ilikuwa na bwawa kubwa la kuogelea. Karibu na bwawa la kuogelea ni gazebo yenye gym na sauna. Kiwanja kina viingilio vitatu na bustani kubwa.

Makao ya familia yake Karen

Iko katikati mwa mtaa wa kitajiri wa Karen jijini Nairobi, lakini katika mwaka wa 2019 haya makao makuu ya familia ya William Ruto yaligeuzwa kuwa nyumba ya kipekee ya wageni.

Ni nyumba ya shilingi milioni nyingi ambayo iko kwenye kipande cha ardhi cha ekari nne, sasa inatumika kama nyumba ya wageni kutoko Hoteli ya Weston.

Jumba la Narok

Inatajwa kuwa makao ya kustaafu ya Mkuu wa Nchi, Rais Ruto. Aliripotiwa kununua Ranchi ya Intona yenye ekari 900 katika Kaunti ya Narok mnamo 2015.

Hii ranchi ina jumba lenye vyumba 35 ambalo linapakana na Hifadhi ya Wanyama ya Maasai Mara.

Amehifadhi mamia ya ng’ombe wa nyama kwenye hii ranchi na ameajiri wafanyikazi wa kusimamia hii shamba.

Nyumba ya Sugoi

Ruto anaendesha shamba la kuvutia katika nyumba yake ya mashambani ya Sugoi, Eldoret, Wasingisu Kaunti. Awali Ruto aliruhusu kamera ndani ya nyumba yake mnamo 2014 wakati wa mahojiano na runinga ya K24.

Ruto alisema kuwa alizaliwa karibu kilomita 10 kutoka alikonunua hii ardhi ambayo anaishi. Ruto alibainisha kuwa shamba hilo lilikuwa na miti mitatu pekee alipoinunua kabla ya kupanda miti 150,000. Pia hapa ndio amefunga kuku zaidi ya 5,000.

Hoteli ya Weston

Iko katika maeneo ya Barabara ya Langata jijini Nairobi na kilomita moja kutoka Uwanja wa Ndege wa Wilson.

Kuna mgahawa wa kifahari, mgahawa wa kawaida na baa ya kisasa. Iko na bwawa la nje, ukumbi wa michezo, sauna na spa.

Comments are closed.