Category: Kamusi

Sehemu hii inahusu maana ya maneno ya Kiswahili na kujifunza kuhusu Lugha ya Kiswahili.

 • Maana ya neno amu na English translation

  Maana ya neno amu Matamshi: /amu/ (Nomino katika ngeli ya [a-wa])  Maana: ndugu wa baba. Kisawe chake ni ami. Amu Katika Kiingereza (English translation) Amu katika Kiingereza ni: Uncle (father’s brother) Read more

 • Maana ya neno amsha na English translation

  Maana ya neno amsha Matamshi: /amsha/ (Kitenzi elekezi) Maana: 1. fanya mtu ashtuke na kufumbua macho kutoka usingizini. 2. zindusha au erevusha juu ya kitu au jambo. Methali: Ukimwamsha aliyelala, utalala wewe: Usifunue siri ya kufanikisha mambo kwa mtu fulani ama sivyo atakuja kukuzidi au kukupita. Mnyambuliko wake ni: → amshana, amshia, amshika, amshwa. Amsha… Read more

 • Maana ya neno amriwa na English translation

  Maana ya neno amriwa Matamshi: /amriwa/ (Kitenzi si elekezi) 1. shurutishwa 2. tendewa uamuzi. Amriwa Katika Kiingereza (English translation) Amriwa katika Kiingereza ni: To be ordered, commanded, decreed, or directed. Read more

 • Maana ya neno amrisho na English translation

  Maana ya neno amrisho Matamshi: /amrifɔ̃/ Wingi wa amrisho ni maamrisho. (Nomino katika ngeli ya [li-ya]) Maana: agizo, shurutisho, hukumu ya amri anayolazimishwa mtu husika kuitekeleza. Amrisho Katika Kiingereza (English translation) Amrisho katika Kiingereza ni: Order, command, decree, or directive. Read more

 • Maana ya neno amrisha na English translation

  Maana ya neno amrisha Matamshi: /amrisha/ (Kitenzi elekezi) Maana: shurutisha amuru au agiza sheria fulani ifuatwe au kutekelezwa. Mnyambuliko wake ni: → amrishana, amrishia amrishika, amrishwa. Amrisha Katika Kiingereza (English translation) Amrisha katika Kiingereza ni:  To order, command, decree, or enforce. Read more

 • Maana ya neno amri na English translation

  Maana ya neno amri Matamshi: /amri/ (Nomino katika ngeli ya [i-zi]) Maana: 1. agizo au tangazo la kuamuru kutekelezwa kwa sheria au jambo fulani. Kisawe chake ni shurutisho. 2. nguvu au uwezo wa mshika hatamu za mamlaka. Amri Katika Kiingereza  (English translation) Amri katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia: Read more

 • Maana ya neno amofasi na English translation

  Maana ya neno amofasi Matamshi: /amɔfasi/ (Kivumishi) Maana: kitu kisicho na umbo au maumbile maalumu. Amofasi Katika Kiingereza (English translation) Amofasi katika Kiingereza ni: Amorphous, shapeless, or formless. Read more

 • Maana ya neno amrawi na English translation

  Maana ya neno amrawi Matamshi: /amrawi/ (Nomino katika ngeli ya [i-zi]) Maana: kamba inayofungwa kwenye pembe moja ya foromali na hutumika pamoja na baraji kusawazisha msukumo wa upepo na mwendo au mwelekeo au jahazi baharini. Amrawi Katika Kiingereza (English translation) Amrawi katika Kiingereza ni: tripping line. Read more

 • Maana ta neno amplifaya na English translation

  Maana ya neno amplifaya Matamshi: /amplifaja/ (Nomino katika ngeli ya [i-zi]) Maana: kifaa cha elektroniki chenye kupaza au kuvumisha sauti. Amplifaya Katika Kiingereza (English translation) Amplifaya katika Kiingereza ni: Amplifier. Read more

 • Maana ya neno ampea na English translation

  Maana ya neno ampea Matamshi: /ampɛa/ (Nomino katika ngeli ya [i-zi]) Maana: pia ampia, kipimo cha mawimbi au mkondo wa umeme. Ampea Katika Kiingereza (English translation) Ampea katika Kiingereza ni: ampere or amp. Read more