Nomino za Makundi/Jamii
Nomino za makundi au jamii ni majina yanayotajia mkusanyiko wa vitu, watu au wanyama.
Mifano ya nomino za makundi
Hizi ni mifano zaidi ya 100 ya nomino za makundi ya watu, vitu na wanyama.
Mifano ya nomino za makundi ya watu
Kikosi cha askari
Mkururo wa watoto
Halaiki ya watu
Mlolongo wa watu
Msafara wa watu
Umati wa watu
Baraza la wazee
Sherehe ya harusi
Baraza la mawaziri
Jamii ya watu
Hadhara ya watu
Sisisi ya watu
Sufufu ya watu
Msafara wa watu
Halmashauri ya shule
Mzengwe wa wagomaji
Kaumu ya watu
Kikoa cha waimbaji
Kilinge cha wachawi
Kilinge cha waganga
Kigaro cha wasingiziaji
Kigaro cha wasengenyaji
Kigaro cha wazushi
Kambi ya wanajeshi
Jopo la waandishi
Paneli ya majaji
Genge la vibarua
Genge la wezi
Sherehe ya mazishi
Sherehe ya kitamaduni
Mifano ya nomino za makundi ya vitu
Shada la maua
Funda la maji
Pakacha la matunda
Jozi ya viatu
Jozi ya soksi
Jozi ya vipuli
Jozi ya karata
Tonge la ugali
Shungi la nywele
Tuta la nywele
Bunda la noti
Bustani la maua
Mkungu wa ndizi
Dazeni ya mayai
Dazeni ya matunda
Dazeni ya vikombe
Taarifa za Habari
Safu ya milima
Seti ya Sahani
Seti ya vikombe
Seti ya fanicha
Sharafa la ndevu
Bunda la karatasi
Biwi la takataka
Biwi la kwekwe
Biwi la magugu
Biwi la simanzi
Doti la leso
Doti la kanga
Mtungo wa maua
Koja la maua
Koja la mawaridi
Kichaa cha matunda
Kichaa cha mboga
Kichaa cha funguo
Chane la ndizi
Chane la nafaka
Chemchemi ya maji
Jaa la takataka
Jaa la magugu
Jaa la kwekwe
Thurea ya nyota
Msitu wa miti
Mlolongo wa magari
Jamii ya miti
Kimba la mavi
Kitita cha kuni
Kichaka cha miti
Shuke la nafaka
Shazi la nafaka
Mnofu wa nyama
Tanuri la chokaa
Tone la damu
Kifurushi cha nguo
Karne ya miaka
Korija ya shanga
Korija ya blanketi
Korija la magunia
Korija la mablanketi
Korija la vitambaa
Kopo la uji
Kopo la chai
Kopo la kahawa
Kanzi la maharagwe
Kanzi la mahindi
Kanzi la ngano
Kanzi la mpunga
Robota la pamba
Robota la mitumba.
Jora la bafta
Jora la vitambaa
Jora la vitenge
Mifano ya nomino za makundi ya wanyama
Zizi la ng’ombe
Mzinga wa nyuki
Bumba la nyuki
Wingu la nzige
Msafara wa siafu
Hombo la samaki.
Mtungo wa samaki.
Tumbi la Samaki
Jamii ya vifaranga
4 responses to “Mifano 100 ya nomino za makundi”