Tashbihi ni lugha inayotumika kulinganisha vitu viwili vinavyofanana au kushabihiana. Inatumia viunganishi mithili ya, kama, mfano wa nk. Hii hap ani mifano ya tashbihi:
Mifano ya tashbihi
- Lala kama mfu
- Ng’ara sawa kama mwezi
- Mwoga mfano wa kunguru
- Simama wima mithili ya dandalo
- Ringa kama tausi
- Lazima kama ibada
- Mweusi mithili ya mkaa
- Mrembo mithili ya Malaika
- Cheka kama radi
- Maridadi kama kipepeo
- Nyeupe Kama theluji
- Mfupi Kama nyundo
- Mfupi kama mbilikimo
- Mrefu Kama mlingoti
- Mrefu kama ngamia
- Mrefu kama twiga
- Mweusi Kama makaa
- Bahati kama mtende
- Nukia kama ruhani
- Nuka kama beberu
- Tamu kama halua
- Nzito kama nanga
- Nyepesi kama unyoya
- Majuto kama ya firauni
- Kuiga kama kasuku.
- Tumainia kama tai
- Baridi kama barafu
- Kigeugeu kama kinyonga
- Mjanja Kama sungura
- Pendana Kama chanda na pete
- Tamu kama asali
- Kali kama Shubiri
- Tengana kama ardhi Na mbingu
- Mnene kama nguruwe
- Pendana kama ulimi na mate
- Polepole kama kobe
- Mweusi kama kizimwili
- Fuata mtu mfano wa kondoo
- Garagara kama mgonjwa
- Kuwa na hakika kama mauti
- Nata kama gundi
- Kuwa imara kama mwamba
- Mlafi kama fisi
- Mwaminifu kama njiwa
- Mjinga kama kondoo
- Mwenye bidii kama mchwa
- Mzima kama kigongo
- Tumbo kama kuruba
- Mkaidi kama punda
- Mkaidi kama kirongwe
- Laini kama hariri
- Laini kama pamba
- Mvumilivu kama mtumwa
- Ganda kama kigaga
- Msiri kama kaburi
- Msiri kama kobe
- Msiri kama usiku
- Msiri kama mvaa buibui
- Nata kama gundi
- Mwembamba kama ufito
- Mwembamba kama Uzi
- Mropokaji kama mlevi
- Baidika kama mbingu na ardhi
- Shabihiana kama kurwa na Doro
- Kigeugeu kama lumbwi
- Mnafiki kama panya
- Kung’aa kama dhahabu
- Angaza kama jua
- Laini kama hariri
- Tamu kama asali
- Nyeusi kama usiku wa manane
- Mrembo kama Malaika
- Jasiri kama simba
- Akili kama mchwa
- Chafu kama fugo
- Cheka kama malaika
- Chanua kama ua la asubuhi
- Chungwa kama mfungwa
- Dahadari kama anayekata roho
- Mwenye bashasha kama mapambazuko
- Mwenye bidii kama mchwa, nyuki
- Mwenye nguvu kama tembo
- Nyingi kama mchanga ufuoni
- Mkali kama simbabuka
- Mwenye maneno mengi kama chiriku
- Tulia kama maji mtungini
- Hasira kama za mkizi
- Fuatana kama kumbikumbi
- Sauti nzuri kama kinanda
- Kuzurura kama mbwakoko
- Kutapatapa kama samaki atolewapo majini
- Mpofu kama jongoo
- Tumbo kubwa kama kiriba.
- Paa kama moshi
- Maneno mengi kama chiriku
- Imara kama chuma cha pua
- Msahaulifu kama Nyati
- Kupenda kama moyo
- Wivu kama joka la mdimu
- Mpole kama kondoo
One response to “Mifano 100 ya tashbihi”