Salamu za kiswahili na majibu

Posted by:

|

On:

|

Kuna salamu nyingi tofauti za kiswahili, kila moja yao ni ya kipekee kulingana na wakati. Hapa chini kuna aina za salamu za kiswahili na wakati wake. Pia kuna salamu za kiswahili pdf mwishoni wa nakala.

Salamu za kiswahili na majibu

Hapa chini utapata maamkizi na majibu.

Aina za salamu na wakati wake

Hapa tumekupa aina za salamu:

  • Salamu za asubuhi
  • Salamu za mchana
  • Salamu za jioni
  • Salamu za usiku
  • Salamu za wakati wowote
  • Salamu za heshima
  • Salamu za pole
  • Salamu za kwaheri
  • Salamu za kuomba msamaha

Salamu za asubuhi

Umeamkaje? – “Salama”.

Salamu ya asubuhi. Inatumiwa kuuliza mtu jinsi alivyoamka siku hiyo.

Sabalkheri? – “Alkheri”.

Salamu ya asubuhi.

Habari za asubuhi – “Njema” au “Nzuri”.

Salamu ya asubuhi.

Chewa – “Chewa”.

Salamu ya asubuhi.

salamu za mchana

Mchana mwema? – “Asante, mchana mwema pia.”

Salamu ya mchana ya kumtakia mtu mchana mwema.

Habari za kutwa? – “Nzuri” au “Njema”.

Salamu ambayo inaweza kutumika wakati wowote wa mchana.

Salamu za jioni

Habari za jioni – “Njema” au “Nzuri”.

Salamu ya jioni.

Masalkheri? – “Alkheri”.

Salamu ya heshima ambayo hutumiwa jioni.

Salamu za wakati wowote

Mambo – “Poa” au “Nzuri”.

Salamu ya wakati wowote.

Shikamoo? – “Marahaba”.

Salamu ya heshima ya wakati wowote.

Salaam aleikum? – “Aleikum salaam”

Ina maana “Amani iwe juu yako”. Salamu hii inaweza kutumika wakati wowote

Habari? – “Njema” au “Nzuri”.

Salamu ya wakati wowote.

Buheri? – “Buheri afya”.

Salamu ya wakati wowote ya kutakia heri njema.

Uhali gani? – “Njema” au “Salama”.

Salamu ya wakati wowote.

Waambaje? – “Sina la kwamba” au “Salama”.

Salamu ya wakati wowote.

Hujambo? –  “Sijambo”.

Salamu ya wakati wowote.

Umeshindaje? – “Salama”.

Salamu ya wakati wowote.

Je, la utu? – “Sina utu”.

Salamu ya wakati wowote.

Cheichei? – “Ewaa”.

Salamu ya wakati wowote.

Karibu tule – “Starehe”.

Salamu inayotumika wakati wa chakula.

Hodi – “Kongoni” au “Karibu”

Hutumiwa wakati mtu anaingia katika nyumba au ofisi, au wakati anaomba kuingia mahali fulani.

Karibu! – “Asante”.

Salamu inayotumiwa kuwakaribisha watu.

Hongera kwa ushindi – “Asante nimehongea”.

Salamu ya kumpongeza mtu.

Salamu za usiku

Alamsiki? – “Alamsiki binuru”.

Salamu ya usiku au ya kupiga kwaheri.

Usiku mwema? – “Asante, usiku mwema pia”.

Salamu inayotumiwa wakati wa usiku.

Lala salama – “Pia nawe” au “Wa salimini”.

Salamu ambayo inatumiwa jioni au usiku kabla ya kulala.

Ndoto Njema – “Za mafanikio”.

Salamu inayotumiwa kabla ya kwenda kulala.

Salamu za kwaheri

Buriani? – “Buriani dawa”.

Hii salamu ina ya  maana ya “kwaheri” au “aheri”  na inatumika wakati wa kupiga kwaheri.

Kwaheri ya kuonana – “Kwaheri ya kuonana”.

Salamu ya wakati wowote, hutumiwa wakati watu wanaagana kwa muda mfupi.

Tuonane tena – “Inshallah” au “Mungu akipenda”.

Salamu ya wakati wowote, hutumiwa wakati watu wanaagana kwa muda mfupi.

Tuonane kesho? – “Majaliwa”.

Salamu ya kuangana hadi kesho.

Salamu za heshima

Mzee, habari? – “Nzuri, mwanangu”.

Salamu ya heshima kwa wanaume wazee inayotumika wakati wowote.

Bwana, habari? – “Nzuri, dada yangu”.

Salamu ya wakati wowote, inatumika kwa watu wazima wa kiume.

Bi., habari? – “Nzuri, kaka yangu”.

Salamu ya wakati wowote, inatumika kwa watu wazima wa kike.

Salamu za pole

Pole kwa ugonjwa – “Asante nimepoa”

Salamu ya kumwambia mgonjwa pole.

Makiwa – “Asante tunayo” au “Asante yamepita”.

Salamu inayotumiwa katika hali ya kusikitisha, hasa katika nyumba ya wafiwa.

Pole – “Nimeshapoa”.

Salamu ya kutoa pole kwa mtu aliyepata shida yoyote, wakati wowote wa siku.

Ugua Pole – “Mungu yupo”.

Salamu inayotumiwa kumtakia mtu anayeumwa apone haraka.

Salamu za kuomba msamaha

Kunradhi – “Niradhi”.

Salamu inayotumiwa kuomba msamaha au kuomba ruhusa.

Niwie Radhi – “Radhi”.

Salamu inayotumiwa kuomba msamaha kwa mtu aliyemkosea.

Samahani – “Umesamehewa” au “Bila Samahani.”

Salamu ya kawaida inayotumiwa kuomba msamaha, wakati wowote.

Salamu za kiswahili pdf

Hapa kuna salamu za kiswahili pdf ya kudownload.

Comments are closed.