Mnyambuliko wa vitenzi na mifano

Mnyambuliko wa vitenzi

Neno mnyambuliko linatokana na kitenzi nyambua lenye maana ya kunyumbua au kurefusha kitu.

Mnyambuliko wa vitenzi ni urefushaji wa vitenzi kwa kuambisha mzizi wa vitenzi kwa viambishi tamati ili kuvipa vitenzi hivyo maana lengwa na halisi.

Kwa mfano kutokana na kitenzi ‘soma’ tunawezapata som-e-a, som-ew-a, som-w-a n.k. Ni vizuri kuelewa kwamba sio vitenzi vyote vinavyonyambulika katika kila kauli.

Kauli za mnyambuliko wa vitenzi

Haja tuaangalia kauli zifuatazo za mnyambuliko wa vitenzi:

  • Kauli ya Kutenda
  • Kauli ya Kutendea
  • Kauli ya Kutendana
  • Kauli ya Kutendeana
  • Kauli ya Kutendwa  
  • Kauli ya Kutendewa
  • Kauli ya Kutendeka
  • Kauli ya Kutendesha
  • Kauli ya Kutendeshana

Kauli ya Kutenda – kitendo katika hali yake ya kawaida (bila kunyambuliwa).

Kauli ya Kutendea – kufanya kitendo kwa niaba(au kwa ajili) ya mtu mwengine.

Kauli ya Kutendana – unamfanya mtu kitendo, naye anakufanya vivyo hivyo.

Kauli ya Kutendeana – unafanya kitendo kwa niaba mtu, naye anafanya kitendo hicho kwa niaba yako.

Kauli ya Kutendwa – kuathirika moja kwa moja na kitendo yaani kupokea moja kwa moja athari ya kitendo.

Kauli ya Kutendewa – kitendo kufanywa kwa niaba yako au kwa ajili yako.

Kauli ya Kutendeka – kitendo kukamilika au kuwa katika hali timilifu.

Kauli ya Kutendesha – kumfanya mtu atende jambo fulani. Kufanyisha.

Kauli ya Kutendeshana – mtu anakufanya utende jambo fulani, nawe unamfanya atende jambo lilo hilo.

Mifano ya mnyambuliko wa vitenzi

TENDATENDEATENDANATENDEANATENDWATENDEWATENDEKATENDESHATENDESHANA
fanyafanyiafanyanafanyianafanywafanyiwafanyikafanyishafanyishana
LimaLimiaLimanaLimianaLimwaLimiwaLimikaLimishaLimishana
PikaPikiaPikanaPikianaPikwaPikiwaPikikaPikishaPikishana
LiaLilia   _Liliana   _   LiliwaLilikaLizaLizana
kulalialanalianaliwaliwalikalishaLishana
pendapendeapendanapendeanapendwapendewapendekapendezapendezana
ombaombeaombanaombeanaombwaombewaombekaombezaombezana
tembeatembeleatembeleanatembeleanatembelewatembelewatembelekatembezatembezana
abuduabudiaabudianaabudianaabudiwaabudiwaabudikaabudishaabudishana
Mifano ya mnyambuliko wa vitenzi

2 responses to “Mnyambuliko wa vitenzi na mifano”

Related Posts