Sauti za Kiswahili ni sauti zinazotumika katika lugha ya Kiswahili. Sauti hizi ndizo zinazounda maneno ya Kiswahili.
Sauti za Kiswahili
Sauti za Kiswahili ni thelathini.
A, B, CH, D, DH, E, F, G, GH, H, I, J, K, L, M, N, NG’, NY, O, P, R, S, SH, T, TH, U, V, W, Y, Z.
Sauti za Kiswahili zinaweza kuainishwa kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:
Aina kuu za sauti
1. Irabu / Vokali(5)
/a/, /e/, /i/, /o/, /u/.
Irabu ni sauti ambazo hutamkwa kwa kufungua kinywa bila kuzuia hewa. Irabu ni sauti zinazounda silabi moja.
2. Konsonanti(25)
/b/, /ch/, /d/, /dh/, /f/, /g/, /gh/, /h/, /j/, /k/, /l/, /m/, /n/, /ng’/, /ny/, /p/, /r/, /s/, /sh/, /t/, /th/, /v/, /w/, /y/ na /z/.
Konsonanti ni sauti ambazo hutamkwa kwa kuzuia hewa sehemu fulani ya kinywa. Konsonanti zinaweza kuwa za sauti au za viziwi.
Konsonanti ni aina mbili.
- Sauti ghuna
- Sauti sighuna
1)Sauti ghuna
Sauti hizi hutamkwa huku nyuzi au glota za sauti zikitikisika. Sauti hizi huwa na mvumo kiasi cha kusikika masikioni zinapotamkwa.
Sauti hizi ni: /b/, /d/, /dh/, /gh/, /ny/, /ng’/, /j/, /v/, /w/, /l/, /r/, /y/, /n/, /g/, /m/ na /z/.
2)Sauti sighuna
Hizi hutamkwa bila mtikisiko wa nyuzi za sauti wala sauti zinazovuma. Hutamkwa kwa ulaini. Sauti hizi ni:
/s/, /ch/, /f/, /h/, /k/, /t/, /p/, /sh/ na /th/.
Aina za sauti na jinsi ya utamshi
Vipasuo
Hutamkwa kwa kukutanisha ala za kutamkia ili kufungilia hewa na kisha kuiachilia ghafla.
Vipasuo ni; /p/, /b/, /k/, /g/, /t/, /d/
Vipasuo sighuna /p/, /k/, /t/ – hutamkwa bila kutikisa nyuzi za sauti.
Vipasuo ghuna /b/, /g/, /d/ – hutamkwa kwa kutikisa nyuzi za sauti.
/p/ na /b/ hutamkwa kwa kukutanisha midomo.
/p/ – papa, pepea, pipi, popo, pua
/b/ – baba, bebea, bibi, bobo, bubu
/t/ na /d/ hutamkwa kwa kukutanisha ufizi na ncha ya ulimi.
/t/ – taa, tetea, titi, toto, tua
/d/ dada, doa, dua
/k/ na /g/ hutamkwa kwa kukutanisha nyuma ya ulimi na kaakaa laini.
/k/ – kaka, koko, kuku
/g/ – gae, gege, gogo, gugu
Vikwamizo/ Vikwaruzo
Pia huitwa Vikwaruzo, hutamkwa kwa kukutanisha ala za matamshi na kisha kuachilia hewa kupitia katika mwanya mwembamba.
Vikwamizo ni; /d/, / f/, /v/, /dh/, /th/, /s/, /z/, /sh/, /h/, /gh/
Vikwamizo sighuna /f/, /th/, /s/, /kh/, /h/, /sh/ – hewa haitikisi nyuzi za sauti.
Vikwamizo ghuna /v/, /dh/, /z/, /gh/ – hewa hutikisa nyuzi za sauti.
/f/ na /v/ hutamkwa kwa kukutanisha mdomo wa chini na wa juu na kuachilia hewa kidogo kupita.
/f/ – faa, fee, fua
/v/ – vaa, vua
/s/ na /z/ hutamkwa kwa kukutanisha sehemu ya kati ya ulimi na kaakaa gumu.
/s/ – sasa, sisi
/z/ – zaa, zeze, zizi, zuzu
/dh/ na /th/ hutamkwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na meno ya juu.
/dh/ – dharau, dhani
/th/ – thubutu
/gh/ na /kh/ hutamkwa kwa kukutanisha kaakaa laini na kilimi.
/dh/ – dharau, dhani
/th/ – thubutu
/h/ hutamkwa kwa kukutanisha kilimi na koo na kuachilia hewa kwa nguvu.
/h/ – haha, hii, huu
Kipasuo-kwamizo: /ch/
Pia huitwa kituo-kwamizo – Hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na ufizi, na kuachilia hewa.
/ch/ – chacha, chechea, choo
Nazali/ Ving’ong’o
Sauti ambazo zikitamkwa hewa hutokea puani.
Nazali ni; /m/, /n/, /ng’/, /ny/
/m/ hutamkwa kwa kukutanisha mdomo wa juu na wa chini, ili kuzuia pumzi kupita kinywani.
/m/ – mama, umeme, mimi,
/n/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na ufizi, ili hewa ipitie puani.
/n/ – nana, nene, nini, nono, nunua
/ny/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na kaakaa gumu.
/ny/ -nyanya, nyuso
/ng’/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na kaakaa laini.
/ng’/ – ng’ang’a, ng’oa
Viyeyusho
Pia huitwa nusu-irabu. Sauti ambazo zinapotamkwa hewa haibanwi wala ala za kutamkia kukutana.
Viyeyusho ni; /y/, na /w/.
/y/ hutamkiwa kwenye kaakaa gumu.
/y/ – yaya, yeye
/w/ hutamkwa midomo ikiwa wazi.
/w/ – wawa, wewe,
Vilainisho/ likwidi
Hizi ni sauti ambazo hutamkwa wakati ala za sauti zinapokaribiana na kutatiza hewa kwa namna maalum. Hutamkwa huku hewa ikiendelea kupita. Kuna aina mbili za likwidi, ambazo ni vitambaza na vimadende.
Kimadende -/r/
Hutamkwa kwa kupigapiga na kukwaruza ufizi haraka haraka kwa ncha ya ulimi.
/r/ – rai, rarua
Kitambaza -/l/
Hutamkwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na ufizi huku hewa ikipitia kwenye pande za ulimi bila kukwaruza ufizi.
/l/ – lala, lea, lilia, lo! lulu
One response to “Sauti zote za Kiswahili na jinsi ya kutamka”