Vitanza ndimi ni maneno yanayokaribiana na kuitanaitana kimatamshi na kumkanganya msomaji hasa anapoyatamka kwa haraka.
Mifano ya vitanza ndimi
- Kanga wa mahanga mwenye matanga anatangatanga tanga.
- Mchuuzi wa mchuzi wa juzi hajui mjusi wa jana.
- Katika kata ya mitakataka mkuu wa kata alikataa katakata takataka zisitupwe pahali tambarare tena.
- Shirika la reli la Seychelles lilishirikiana na shirika la reli la Senegal.
- Wape wale wanawali wale wali wao.
- Pema ni pema hujapopema ukipema si pema tena.
- Ni Nini kikusikitishacho?
- Kisikitiko kikusikitikisacho kisikitie.
- Msasa wa sasa wa Sasha una mkasa wa kasa si kasha.
- Susumila Shushushu mwenye sunzu si zuzu ila ana susu yenye shushu na ni chuchu.
- Ukivumbua alichovumbua Wambua akila kitumbua bila kukichambua sitakusumbua tena.
- Katibu Kata wa kata ya mkata alikataa katakata kukatakata takataka zilizokuwemo katika kata ya mkata.
- Mpambe mpeleke pembeni apambike ajue pembea ni mbeya.
- Bw Karama amaeandaa karamu iliomgarimu gharama kubwa.
- Baba alivua papa mkubwa baharini baada ya mvua kubwa kunyesha.
- Biketi aliketia kiketi alipofika kwa Keti wa Bi. Keti.
- Wali wa Liwali umeliwa na wana wa Liwali.
- Wale watu wa Liwali wala wali wa Liwali.
- Wanawali wa awali hawali wali wa awali ila wali wao.
- Nyanya Tanya alimkanya Tanya kutotawanya nyaya za nyanya ndani ya kaya.
- Shangaa kama shangazi aliyeshangaa baada ya kupoteza shanga kule tanga.
- Usishangae kama shangazi aliye nunua shanga kwa bei ya kushangaza.
- Wataita wa Taita wataita Wataita wa Taita.
- Sitasita kusisitisa kuwa sita na sita si tisa.
- Paliondokea mamba aliejibamba na kujigamba katika magamba ya wakamba huko ukambani.