Kampuni za kupeana pikipiki za mkopo Kenya

Nchini Kenya bei ya boda boda mpya ni zaidi ya Ksh. 80,000. Ikiwa huna pesa hizo, usijali, kwa sababu katika makala hii tutakuonyesha jinsi ya kupata pikipiki ya mkopo nchini Kenya.

Kampuni za kupeana mkopo wa pikipiki

MOGO

MOGO hutoa ufadhili wa bei nafuu kwa magari yaliyotumika, Boda Boda na mikopo ya Tuk Tuk.

Jinsi ya kupata mkopo wa Boda Boda kutoka MOGO.

Ili kupata mkopo wa pikipiki kutoka MOGO, unahitaji kufikia vigezo hivi:

  • Malipo ya kwanza ya asilimia ishirini (20%).
  • Taarifa ya M-PESA ya miezi sita (M-PESA statement).
  • Kitambulisho cha taifa.
  • KRA Pin.
  • Uwe na umri wa miaka 20-65.
  • Mdhamini mmoja. (guarantor).
Umuhimu wa kupata mkopo wa pikipiki kutoka MOGO
  • Unalipia kutoka kiwago Kidogo kama KES 259 kwa siku.
  • Unachagua aina yoyote ya pikipiki na unaaza kuendesha siku hiyo.

Watu

Watu ni kampuni inayosaidia mamilioni ya watu barani Afrika kutimiza ndoto zao za kuwa wajasiriamali. Pia ni mojawapo ya makampuni inayoongoza kwa kutoa mikopo ya pikipiki nchini Kenya.

Mahitaji ndio upate mkopo wa pikipiki kutoka Watu

Ili kuhitimu kupata mkopo wa boda boda kutoka kampuni ya Watu, unahitaji kuwa na:

  • Kitambulisho cha taifa.
  • KRA pin.
  • Malipo ya kwanza kwa pikipiki utakayochagua.
  • Mdhamini mmoja (guarantor).
  • Two referees – watu ambao umefanyia kazi na wanakujua vizuri sana.
  • Nambari ya simu ya Safaricom ambayo imesajiliwa kwa M-Pesa na imekuwa ikitumika kwa miezi sita iliyopita.

Mwananchi Credit Limited

Mwananchi Credit Limited ni kampuni nchini Kenya inayopeana mikopo ya pikipiki na Tuktuk nchini Kenya.

Mahitaji ndio upate mkopo wa pikipiki kutoka Mwananchi Credit Limited

Ili kupata mkopo wa pikipiki kutoka Mwananchi Credit unastahili kuwa na:

  • Picha ya pasipoti .
  • Nakala ya kitambulisho.
  • Nakala ya Pin ya KRA.
  • Taarifa Iliyothibitishwa ya M-Pesa kwa miezi sita. (M-PESA statement).
  • Wadhamini watatu na nakala za kitambulisho zao, mdhamini mmoja awe jamaa wa karibu.
  • Malipo ya kwanza ya KES.15,000, pia inajulikana kama ada ya ahadi.
Umuhimu wa Mwananchi Credit
  • Unapata bima ya kina ya pikipiki.
  • Pikipiki itakuwa na ‘tracking device’- kifaa cha kufuatilia pikipiki mahali inaenda.
  • Malipo ya chini ya kila siku ya KES 300.
  • Muda mrefu wa ulipaji wa mkopo (miezi 18).

KCB

KCB inatoa mikopo ya pikipiki kwa kufadhili asilimia sabini (70%) ya gharama ya pikipiki. Kwa hivyo 30% nyingine unahitaji kuitafuta.

Mahitaji ndio upate mkopo wa pikipiki kutoka KCB

  • Akaunti inayotumika ya taasisi yoyote ya biashara ambapo mapato ya biashara yanatumwa kwa angalau miezi tatu.
  • Proforma invoice kutoka kwa wauzaji wa Boda Boda na Tuk Tuk.
  • Leseni ya kuendesha boda boda.
  • Uwezo wako wa kurejesha mkopo
  • Benki itafadhili hadi 70% huku mteja atakidhi 30% ya gharama.
  • Mdhamini mwenye ako na akaunti ya KCB.
  • KCB bank statement ya miezi sita au akiba ya chama ya miezi tatu.

Viwango vya mikopo na ada ya KCB:

  • KCB Base rate 13% per annum.
  • Negotiation fee – 3%.

Progressive credit

Progressive credit inalenga kuwawezesha wamiliki wa boda boda kupata mikopo ya biashara, mikopo ya karo za shule, mikopo ya dharura, utengenezaji wa pikipiki au kupata pikipiki mpya.

Mahitaji yakupata mikopo ya boda boda kutoka kwa Progressive credit.

  • Kitambulisho taifa.
  • KRA pin.
  • Mdhamini mmoja.
Umuhimu wa Progressive credit
  • Utapata access to mobile loans.
  • Free helmet.
  • Bima ya maisha.
Related Posts