William Kipchirchir Samoei arap Ruto (aliyezaliwa 21 Desemba 1966, Sambut, Kenya) ni mwanasiasa wa Kenya ambaye amehudumu kama rais wa tano wa Kenya tangu 13 Septemba 2022. Kabla ya kuwa rais, aliwahi kuwa naibu wa rais wa kwanza wa Kenya kutoka 2013 hadi 2022.
Mali ya William Ruto
Kufikia 2023, ripoti zinaonyesha kuwa thamani ya mali ya William Ruto inakadiriwa kufikia takriban Ksh. bilioni 40. Utajiri huu mkubwa umepatikana kupitia ushiriki wake katika siasa, na uwekezaji katika biashara mbalimbali kama vile kilimo na hoteli.
Haya ni baadhi ya mali ghali yanayomilikiwa na William Ruto:
- Ako na thamani ya Ksh. bilioni 2.5 kwa kampuni ya Orterter Enterprises Limited.
- Mali za Makazi kando ya Barabara ya Jogoo yanayokadiriwa kwa thamani ya Ksh. bilioni 1.5.
- Hoteli ya Weston katika Uwanja wa Ndege wa Wilson inayokadiriwa kwa thamani ya Ksh. bilioni 2
- Ghorofa ya Osere katika mtaa wa Ongata Rongai katika Kaunti ya Kajiado inayokadiriwa kwa thamani ya Ksh. milioni 500.
- Biashara ya kuku huko nyumbani kwao Uasin Gishu inayokadiriwa kwa thamani ya Ksh. milioni 750
- Kampuni ya Bima ya Amaco inayokadiriwa kwa mamilioni.
- Hoteli ya ghorofa yenye thamani ya Ksh 3 Bilioni jijini huko Nairobi CBD.
- Helikopta tatu za Eurocopter huku kila moja ikigharimu takriban Ksh. milioni 300.
- Nyumba na mashamba ya Uasin Gishu ya ekari 700 yenye thamani ya Ksh. bilioni 1.2.
- Saa ya mkononi ya dhahabu inayokadiriwa kwa Ksh. milioni 2.6.
- Kituo cha TV cha K24 alichonunua kutoka kwa familia ya Kenyatta.
- Gari la Lexus LX570 lenye thamani ya Ksh. milioni 35.
- Ako na Ksh. 1 bilioni kwa kampuni ya Oseng Property Limited.
- Gari la Range rover la mamilioni.
- Ruto pia anamiliki ekari 15,000 za ardhi huko Laikipia, ekari 976 katika shamba la Murumbi huko Trans Mara, na ekari 2,536 huko Taita Taveta.
- Kama rais wa Kenya William Ruto anapokea mshahara wa zaidi ya Ksh. milioni 29 kwa mwaka (hii ni pamoja na posho).