Hapa kuna Sauti Ya Watu Lyrics by Ney Wa Mitego. Mwishoni utapata ujumbe muhimu unaowasilishwa na wimbo huu.
Ney Wa Mitego: Sauti Ya Watu Lyrics
Hii sio sauti ya kiharakati, wala
Ukombozi wa musa na fimbo yake
Bali haya ni maumivu ya mnyonge
Anaye wakilisha walala hoi wenzake
Kwenye kinywa kilicho kosa
Pa kusemea hisia zake
Natanguliza samahani kwa wale nitakao wakwaza
Yamenifika hapa nimeshaidwa kunyamaza
Wapo wengi kama mimi wenye sauti kama mimi
Sijui ni ubinafsi hawasemi kama mimi
Anko alisema kwamba tuko uchumi wakati
Haya tudanganyeni tena tupo uchumi wa ngapi
Wapigaji waliotumbuliwa ndio wamerudi mzigoni
Kameadi ka million mnataja mabilioni damn
Amna huruma ninyi na sisi masikini
Hivi hio bajeti si mngeweka hospitalini
Na huyu ndio Yule binti aliemaliza chuo
Ila uakka wakazi aliyosomea uko chuo
Hajua atafanya nini amebaki na vyeti vyake
Anajuta alisoma nini si angejiuza ka wenzake
Panya road jina la pili la kijana asiekua na ajira
Na risasi ndio hukumu inamfika hata asie na hatia
Hakuna uafadhari wa maisha vyuma vimezidi kukaza
Mambo yanaharibika na wapinzani wamenyamaza
Kama ulimpenda baba huwezi mwelewa mama
Na kama hukumpеnda baba bado utamchukia mama
Yani kumpenda mama na kumchukia baba ni sawa
Kuipenda nyama halafu upendi mchuzi wakе
Mmmh, hii ni sauti ya watu
(Na hili giza tunaenda wapi
Tunafanya nini
Tutaishi vipi
Hata mwanga hauonekani)
Ukiona mtoto halii njaa na nyumbani hakuna chakula
We mchunguze vizuri kuna sehemu anakula
Mwambieni ukweli mama hali mbaya sio tandale sio masaki
Kilio cha kila mtu pesa hakuna imefichwa wapi
Siku hizi mpaka vigenge vya nyanya TRA wanataka kodi
Masikini amejichanga vipesa benki anakatwa tozo
Hizo V8 mnazonunua si hela zetu za kodi
Naona mna enjoy kuliko hata walipa kodi
Mnajenga hospitali madawa hakuna
Mnatujengea shule lakini walimu hatuna
Kudanga ndio kimbilio kubwa la dada zetu
Ndio mtaji asiokopeshwa hakatwi tozo wala kodi
Hivi mnaakili nyinyi mnashauri tujiajiri
Wakati nyinyi wenyewe mpaka sasa mmeajiriwa
Achieni nafasi zenu nanyinyi mkajiajiri
Hapo ndipo nitapoamini kweri nyie washauri wazuri
Kati ya mtawala na mpinzani hapa muogo nani
Mtawala aliekataza mikutano isifanyike
Au mpinzani asieifanya na anajua ni haki yake
Mmmh, hii ni sauti ya watu
(Na hili giza tunaenda wapi
Tunafanya nini
Tutaishi vipi
Hata mwanga hauonekani)
He he he
Bi mkubwa anapambana sana
Pengine hofu ni kuhusu swali la msingi kwenye vijiwe vyetu
Je vita yake na anaowaamini ni sawa
Zisije zikawa ni mbili tofauti
Tumerudi kule kule
Maji ya mgao umeme mgao
Maji hayatoki bili zinatoka
Mmmh, polisi hongereni kwa jitihada nyingi
Hamsemwi kwa ubaya lakini pia hamsingiziwi
Acha iendelee kunyesha tuone panapovuja
Jumbe za kujifunza kutoka kwa “Ney Wa Mitego: Sauti Ya Watu”
Maneno ya wimbo huu yanawasilisha ujumbe kadhaa, zikiwemo changamoto za kijamii na kiuchumi, mapambano ya watu wa kawaida, na wito wa uwajibikaji. Hapa kuna baadhi ya ujumbe uliotolewa kutoka kwa wimbo huu:
Mapambano ya kijamii na kiuchumi
“Hii sio sauti ya kiharakati, wala Ukombozi wa Musa na fimbo yake. Bali haya ni maumivu ya mnyonge, Anaye wakilisha walala hoi wenzake.”
Maneno haya yanaangazia mapambano na maumivu ya kila siku ya watu wasio na uwezo katika jamii, yakiwakilisha sauti ya waliokandamizwa.
Wito wa uwajibikaji na uwazi
“Wapigaji waliotumbuliwa ndio wamerudi mzigoni, Kameadi ka million mnataja mabilioni damn. Amna huruma ninyi na sisi masikini.”
Maneno haya yakosoa ufisadi na ukosefu wa huruma kwa maskini, yakitilia shaka mgao wa fedha na rasilimali.
Changamoto wanazokumbana nazo vijana
“Panya road jina la pili la kijana asiekua na ajira. Na risasi ndio hukumu inamfika hata asiye na hatia.”
Maneno haya yanazungumzia changamoto zinazowakabili vijana, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira na matokeo mabaya wanayoweza kukabiliana nayo.
Ukosoaji wa kisiasa na maoni ya kijamii
“Kati ya mtawala na mpinzani hapa muogo nani. Mtawala aliekataza mikutano isifanyike. Au mpinzani asieifanya na anajua ni haki yake.”
Maneno hayo yanawakosoa watawala na viongozi wa upinzani, yakitilia shaka kujitolea kwao kwa maadili ya kidemokrasia na haki za raia.
Uwezeshaji na kujitegemea
“Hivi mnaakili nyinyi mnashauri tujiajiri. Wakati nyinyi wenyewe mpaka sasa mmeajiriwa.”
Maneno haya yanapinga ushauri wa kujiajiri wakati wale wanaotoa ushauri mara nyingi wameajiriwa wenyewe, wakitaka fursa za uwezeshaji za kweli.