Ikiwa unajaribu kuondoa mafuta ya tumbo karibu na kiuno chako, jaribu vyakula hivi:
Vyakula na jinsi ya kupunguza tumbo
Tumia pilipili manga
Pilipili Manga (black pepper); hiki ni kiungo kilicho katika mbegu ndogondogo nyeusi, ambazo zina ladha ya pilipili.
Kama viungo vingine, pilipili manga inatumika katika mapishi kuongeza ladha ya chakula, kuleta harufu nzuri na kukifanya chakula kichangamke.
Unaweza kuweka pilipili manga kwenye supu, chai, uji, samaki, nyama na hata mboga.
Pilipili manga ina vitamini nyingi ila kuu ni A, E na K na madini mfano calcium, zinc, copper, magnesium nk. Kuongeza pilipili manga kwenye mlo wako pamoja na mazoezi sahihi na mlo wa afya bora kutasaidia kuchoma mafuta ya tumbo haraka.
Mananasi
Mananasi ni tamu na pia iko na virutubisho kadhaa. Protini, madini na vitamini katika mananasi vinaweza kusaidia kupunguza uzito na kupunguza mafuta ya tumbo.
Sasa basi, fuata ratiba hii kama unatumia nanasi:
ASUBUHI
- Anza siku yako kwa kunywa maji, iwe ya vuguvugu au ya kawaida, ila si baridi. Inaweza kuwa nusu lita au zaidi.
- Kula mihogo au viazi, magimbi, maboga, au ndizi za kuchemsha kiasi, pamoja na kachumbari.
- Kama utapata kitoweo, basi kula hata mayai ya kuchemsha au kukaanga bila mafuta.
- Kunywa na ukwaju au ubuyu wa kuchemsha.
N.B. Zingatia: Inashauriwa kula kwa kushiba na kunywa maji ya kutosha. Kufanya hivi asubuhi huleta matokeo mazuri ya kupungua na kiafya kwa ujumla.
MCHANA
Kula nanasi nusu, hifadhi nusu nyingine ule jioni. Pia usikose kunywa maji kulingana na kilo zako.
Ukifanya hivi kwa wiki moja bila ya kula vitu vingine kama vya sukari na mafuta, basi utaanza kuona mabadiliko ya kupungua kwa tumbo lako.
Pia unaruhusiwa kuendelea kula hivi kwa kula matunda tofauti tofauti. Kama utajihisi umepungua sana, basi mchana utajumuisha baadhi ya vyakula ulivyokula asubuhi, japo kwa uchache sana.
Tumia Tangawizi
Tangawizi huyeyusha mafuta. Tangawizi husaidia kupunguza kuganda kwa mafuta mwilini ambayo yana madhara makubwa mwilini, Hasa magonjwa ya kiharusi na shinikizo la damu. Utafiti unaonyesha kuwa kuweka sukari ya damu thabiti inaweza kusaidia kupunguza tumbo na uzito kwa ujumla.
Juisi ya kutoa sumu mwilini na kupunguza tumbo
Mahitaji:
- Tango 1
- Limau 1
- Fundu moja la majani ya kotimiri (giligilani)
- Tangawizi mbichi kijiko 1
- Maji safi 1/2 lita
Maelekezo:
- Osha vizuri tango na kotimiri.
- Safisha vizuri tangawizi na uisage kwenye kisagio. Kiasi kiwe kijiko kimoja tu.
- Weka vitu vyote kasoro limao kwenye blenda na saga vizuri. Unaweza kuchuja au kunywa hivyo hivyo.
- Ukishasaga juice yako, kamulia limao.
- Kunywa.
Faida:
- Juice hii ni nzuri ukinywa usiku unapoenda kulala.
- Ni kinywaji kinachotoa sumu zote mwilini na kupunguza tumbo.
Kula vyakula vya protini
Vyakula vya juu vya protini, kama vile samaki, nyama, na maharagwe, vinaweza kuwa na manufaa ikiwa unajaribu kupunguza mafuta ya tumbo.
Hakikisha kila mlo wako una protein, kuanzia chakula cha asubuhi.
Mfano wa vyakula vyenye protini:
- Nyama: Ya ng’ombe, kuku, mbuzi n.k
- Samaki: Salmon, sato, sangara, prawns n.k
- Mayai: Ya kuku wa kienyeji ni mazuri zaidi
- Mbegu na karanga: Mbegu za chia, karanga za almonds
Punguza sukari na ulaji wa wanga
Ulaji mwingi wa wanga unahusishwa na mafuta mengi ya tumbo. Zingatia kupunguza ulaji wako wa vyakula vya wanga vilivyotenegenzwa na makambuni na hubadilisha kwa wanga safi katika mlo, vyanzo vya afya vya wanga, ni kama vile nafaka nzima, kunde, au mboga.
Pia ulaji wa sukari kupita kiasi ni sababu kuu ya kuongezeka uzito kwa watu wengi. Punguza ulaji wako wa peremende na vyakula vilivyochakatwa vilivyo na sukari nyingi.
Vidokezo vingine vya kupunguza tumbo
Punguza msongo wa mawazo (Stress)
Stress zinaweza kukuza kuongezeka kwa mafuta karibu na kiuno chako. Kupunguza mafadhaiko yako kunapaswa kuwa moja ya vipaumbele vyako ikiwa unajaribu kupunguza uzito.
Utafiti unaonyesha kuwa viwango vya juu vya stress huongeza hamu ya kula na huendesha uhifadhi wa mafuta ya tumbo.
Fanya mazoezi
Mazoezi ni njia bora ya kupoteza uzito. Utafiti unaonyesha kuwa mazoezi ni bora sana katika kupunguza mafuta ya tumbo na mafuta ya mwili kwa ujumla. Kama hauwezi kunyanyua uzito basi unaweza kufanya mazoezi ya cardio kama jogging,kuendesha baiskeli, kuogelea, zumba nk.