Hapa kuna “Haijakaa Sawa Lyrics” by Mbosso. Mwishoni utapata jumbe za kumfariji mpenzi na kumpa matumaini kutoka kwa huu wimbo.
Mbosso: Haijakaa Sawa Lyrics
Sasa unanuna nini?
Au unadhani hata mimi napenda
Nishazichoka na mimi
Mboga za majani kila siku mlenda
Siko juu siko chini
Niko nusu sadoo
Sio wa kumi si sabini
Ngoma ngumu bado
Kama ibada naswali sana
Usiku wa manane
Tena nafunga na Suna
Mambo bado bado mwana wane
Naona yanazidi kuguma
Nikirudi na hasira hasira (nizoee)
Mambo magumu bado bila bila (niombee)
Nikirudi na hasira hasira (nizoee)
Mambo magumu bado bila bila (niombee)
Halijakaa sawa
Nivumilie ipo siku tutapata
Halijakaa sawa
Shida na dhiki zitakwisha baby
Halijakaa sawa
Kuchana kope make up utapaka
Halijakaa sawa
Tutabadili mboga kuku kwa manyama
Chochea kuni kipenzi changu
Asubuhi tumbo likikuming’inya
Pokea kidogo changu
Tunywe chai na mkate wa kumimina
Akili ikichoka riziki nikikosa
Najua kwako nitajiliwaza
Kama makosa nivute chumbani
Kununa nuna unajilemaza
Ustahimilivu mnao wachache mno
Jua shida rafiki wa mbivu
Baada ya dhiki mavuno
Kila jema lina maumivu
Na kwenye waliopo tumo
Yarabi salama tupe tulivu
Penzi lisifike kikomo
Iyee eeh eeh
Nikirudi na hasira hasira (nizoee)
Mambo magumu bado bila bila (niombee)
Nikirudi na hasira hasira (nizoee)
Mambo magumu bado bila bila (niombee)
Halijakaa sawa
Nivumilie ipo siku tutapata
Halijakaa sawa
Shida na dhiki zitakwisha baby
Halijakaa sawa
Kuchana kope make up utapaka
Halijakaa sawa
Tutabadili mboga kuku kwa manyama
Maneno ya kumfariji mpenzi kutoka kwa “Mbosso: Haijakaa Sawa Lyrics”
- Mambo bado mwana, naona yanazidi kuguma. Nikirudi na hasira nizoee, mambo magumu bado naomba uniombee.
- Mambo bado sawa, nivumilie ipo siku tutapata na shida na dhiki zitakwisha baby.
- Akili ikichoka riziki nikikosa najua kwako nitajiliwaza.
- Jua shida rafiki wa mbivu, baada ya dhiki mavuno, kila jema lina maumivu.
- Na kwenye waliopo tumo, Yarabi salama tupe tulivu, penzi lisifike kikomo.