Maana ya neno sawa – Sawa meaning in Kiswahili
Ni neno linaweza kutumika katika hali mbalimbali ili kueleza makubaliano, uelewa, kukubalika, au uzuri..
Visawe vya sawa
- Barabara
- Ndiyo
Sawa in English
Neno “sawa” linaweza kuwa na maana mbalimbali katika Kiingereza (English), kulingana na muktadha. Hapa kuna baadhi ya tafsiri za kawaida kwa Kiingereza:
Okay
Neno hili hutumika kuonyesha kukubaliana au kukubali.
Mfano wa sentensi:
“Okay, it’s no problem. I’ll come tomorrow.” – Sawa, haina shida. Nitakuja kesho.
Fine
Neno hili linamaanisha kuwa kitu ni kizuri au cha kuridhisha.
Mfano wa sentensi:
“Our relationship is fine” – “Uhusiano wetu uko sawa”
All right
Neno hili linamaanisha kuwa kitu fulani ni cha ubora wa kuridhisha au unaokubalika.
Mfano wa sentensi:
“The tea was all right” – “Chai ilikuwa sawa”
Acceptable
Neno hili linamaanisha: kuweza kuafikiwa au inafaa
Mfano wa sentensi:
“Her explanation was clear and acceptable.” – Maelezo yake yalikuwa wazi na kukubalika.
Kwa ujumla neno sawa katika Kiingereza, linaweza kutafsiriwa kama okay, fine, all right, au acceptable.