Matumizi ya kiambishi -KA-

Kiambishi KA

Kiambishi ni kisehemu au kipashio ambacho huongezewa mzizi wa neno ili kulipa maana zaidi au kubadili aina ya neno katika kuunda neno jipya.

Kiambishi KA hutumiwa kuonyesha mfululizo wa vitenzi katika wakati uliopita,usemi halisi, wakati usiodhihirika, kuhimiza/kupendekeza, kuamrisha na kuonyesha matokeo ya kitendo kilichotangulia.

Matumizi ya -KA-

Hutumika Kuonesha;

a) Mfufulizo wa vitendo – Kufanyiwa kwa vitendo kwa kufuatana.

Mama alifika sebuleni akawasha runinga,akaanza kusikiliza matokeo ya uraisi.

Nilikwenda kijijini nikamwona mwalimu wangu, nikamsalimia na nikamwomba aje nami jijini Bujumbura akakubali.

Tulifika nyumbani, baba akatuuliza tumewaacha wapi fahali.

Alikula akashiba kisha akalala.

b) Amri/shuruti/ kuagiza/ kuamuru

Kalime shamba lile.

“Kalaleni!”Mama akawaamuru.

Kamwambie asirudi hapa tena!

Kamwambie!

c) Sababu/dhamira/ matarajio/Nia ya kutenda jambo.

Alienda shuleni akasome Kiswahili.

Naomba fedha nikanunue vitabu.

d) Wakati usiodhihirika

Mwalimu akamtuma mwanafunzi karo.

Mama akamtuma mwanawe aende kuchota maji.

Nikamwuliza anionyeshe sanduku lake.

e) Kitendo kimoja ni tokeo la kingine

Omanyala alikimbia vyema akatuzwa.

f) Kiishio cha kauli ya kutendeka

Kijana mtundu alipigwa akapigika.

Ulijaribu kufungua mlango lakini haukufunguka.

g) hutumiwa katika hali ya ombi

Twende tukale!

Matumizi ya kiambishi -KA- katika senetnsi

Mifano ya kubainisha matumizi ya KA katika sentensi:

Musya ameenda mtoni akachote maji. – Hapa ‘ka’ imetumika kama kiambishi cha kuonyesha sababu.

Tulifanya mazoezi tukashinda. – Hapa ‘ka’ imetumika kama kimabishi cha mfuatano wa matukio.

Atakayenitembelea. – Hapa ‘ka’ inarejelea hali mbili:

1.Wakati ujao: Hakuna wakati wowote unaoweza kutumia KA isipokuwa Wakati ujao.

2.Kirejeshi nafsi hasa ya tatu (yeye).

Mumbi alitia embe kapuni likaiva. – Ka ya kwanza imetumika kuonyesha sehemu embe lilipoekwa, ka ya mbili inaonyesha mfuatano wa vitendo (Kutia na kuiva).

Related Posts