Ngeli ya U-YA na Mifano

Ngeli ya U-YA huwa na majina ya hali, matendo, na kadhalika. Kiambishi {–u} katika umoja na {–ya} katika wingi hutumika katika upatanisho wake wa kisarufi.

Mfano:

Upishi wake «u»mewavutia.

Mapishi yake «ya»mewavutia.

Miundo ya ngeli ya U-YA.

U-MA: Ugonjwa – magonjwa, upana-mapana, uovu-maovu

Nomino katika ngeli ya U-YA

Ugonjwa-magonjwa

Umbo-maumbo

Uwele-mawele

Unyoya-manyoya

Ubele-mabele

Ubua – mabua

Ubele – mabele

Upishi – mapishi

Ulezi —malezi

Uovu-maovu

Ua – maua

Mfano katika sentensi

  • Ugonjwa wa moyo unaweza kusababisha kifo. – Magonjwa ya moyo yanaweza kusababisha kifo.
  • Umbo la gari hili ni la kuvutia. – Maumbo ya magari haya ni ya kuvutia.
  • Uwele ni ugonjwa. – Mawele ni magonjwa.
  • Unyoya wa ndege ni laini. – Manyoya ya ndege ni laini.
  • Upishi wa chakula cha kienyeji ni tamu. – Mapishi ya vyakula vya kienyeji ni matamu.
Related Posts