Though in Swahili (English to Swahili Translation)

Though definition in English

Indicates that a factor qualifies or imposes restrictions on what was said previously.

Though in Swahili

Though in Swahili is translated as: ingawa, ijapo, ijapokuwa, walau, hata kama or lakini.

Examples of though in Swahili in sentences

  • Niko hai ingawa sioni dalili zozote za uhai. (I am alive even though I am not showing any signs of life.)
  • Unaonekana kana kwamba hakuna kitu kilichotokea kwako. ( You look as though nothing has happened to you.)
  • Ijapo ninakubali unachosema, bado naona unakosea.  (Though I admit what you say, I still think you are wrong.)
  • Ingawa ni tajiri, hana furaha. (Even though she is rich, she is not happy.)
  • Hata kama haikuwaimekamilika, alimaliza kuandika maandishi yake. ( Even though it was not perfect, he finished writing his manuscript.)
  • Hata kama alikimbia, mzee huyo alikosa treni ya mwisho.  (Even though she rushed, the elderly woman missed the last train.)
  • Nilihisi kulikuwa na kitu cha ajabu, lakini sikujua ni nini.  (I felt there was something strange, but I didn’t know what.)
  • Ingawa ilikuwa baridi, hakuwasha moto.  (Though it was cold, he didn’t light the fire.)
  • Ingawa anaishi karibu na shule, mara nyingi anachelewa. (Though he lives nearby and the school is close, he is often late.)
  • Cha kushangaza ni kwamba taa zote za ndani ya nyumba zilikuwa zimewaka, ingawa hakukuwa na mtu nyumbani. (Surprisingly, all the lights inside the house were on, even though no one was home.)
  • Alifaulu mtihani wa kuendesha gari hata kama alikuwa dereva mbaya.  (He passed the driving test even though he was a bad driver.)
  • Ingawa mvua ilisimama, upepo ulikuwa bado unavuma kwa nguvu.  (Even though the rain stopped, the wind was still blowing strongly.)
  • Ingawa ilikuwa inanyesha, alitoka nje. (Even though it was raining, she went out.)
  • Ingawa ilikuwa inanyesha, tulicheza mpira wa miguu.  (Even though it was raining, we played football.)
  • Waliendelea na matembezi, ingawa ilinyesha. (They continued with the stroll, even though it was raining.)
  • Ingawa alitamani kusafiri nje ya nchi peke yake, alibadili mawazo.  (Even though she wanted to travel abroad alone, she changed her mind.)
  • Ingawa daktari alijitahidi, kupona kwa mgonjwa kulichelewa.  (Even though the doctor tried, the patient’s recovery was delayed.)
  • Alishikilia maoni yake ingawa nilimweleza asifanye hivyo.  (He stuck to his opinion even though I told him not to.)
  • Ingawa alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili tu, Violet alijua jinsi ya kujipatia riziki. (Even though she was only twelve years old, Violet knew how to make a living.)
  • Ingawa Charlie anapenda kazi yake sana, hailipi vizuri.  (Though Charlie loves his job, it doesn’t pay well.)
  • Zach hakuwa mnyonge ingawa alikuwa tajiri.  (Zach wasn’t weak even though he was rich.)
  • Ingawa nilikuwa nimekaa kwa jua, bado nilijisikia baridi.  (Even though I was sitting in the sun, I still felt cold.)
  • Ingawa nimeamua kwenda kwenye sherehe, sitarajii.  (Even though I’ve decided to go to the party, I’m not looking forward to it.)
  • Ingawa Sali ni Mtanzania, hawezi kuongea Kiswahili.  (Even though Sali is Tanzanian, she can’t speak Swahili.)
  • Ingawa alikuwa na shughuli nyingi, alikuja kunisalimia.  (Even though she was busy, she came to greet me.)
  • Ingawa ilikuwa tayari ni jioni sana, aliendelea kufanya kazi. (Even though it was already very late, he continued working.)
  • Ingawa ilikuwa baridi sana, nilitoka nje.  (Even though it was very cold, I went outside.)
  • Kwa nini ananitazama kana kwamba ananijua?  (Why is he looking at me as though he knows me?)
  • Ina harufu kana kwamba mtu amekuwa akivuta sigara hapa.  (It smells as though someone has been smoking here.)
  • Ingawa nilikuwa sahihi, alishinda.  (Even though I was right, he won.)
  • Ingawa amesoma, siwezi kumheshimu.  (Even though he’s educated, I can’t respect him.)
  • Ingawa inanyesha, haijali hata kidogo.  (Even though it’s raining, it doesn’t care at all.)
  • Ingawa hupendi hii, lazima uile. (Even though you don’t like it, you must eat it.)
  • Niliachana na gari langu la zamani, ingawa nilichukia kufanya hivyo.  (I parted with my old car, though I hated to do so.)
  • Bwana Mike hajatokea bado ingawa aliahidi kuja.  (Mr. Mike hasn’t shown up yet, even though he promised to come.)
  • Ingawa Bwana Bob alikuwa tajiri sana, alikuwa mchoyo.  (Even though Mr. Bob was very wealthy, he was stingy.)
  • Hata kama Jim anafanya kazi kwa bidii sana, kazi yake hailipi vizuri sana.  (Even though Jim works very hard, his job doesn’t pay very well.)
  • Ingawa Jane si mkimbiaji mzuri, anaweza kuogelea kwa kasi sana.  (Even though Jane is not a good runner, she can swim very fast.)
Related Posts