Ukucha ni sehemu ndogo ngumu ya mwili mfano wa pembe inayoota kwenye kidole cha binadamu, mnyama au ndege.
Wingi wa ukucha
Wingi wa ukucha ni kucha.
Kucha ni kadha za vidole, wingi wa ukucha.
Mfano: Nimekata kucha zote ndefu katika vidole vyangu.
Umoja wa kucha
Umoja wa kucha ni ukucha.
Mfano: Nimekata ukucha ndefu wa kidole changu.
Mifano ya umoja na wingi wa ukucha katika sentensi
- Niliikwangua rangi kidogo kwa ukucha. (Walikwangua rangi kidogo kwa kucha.)
- Nilivunja ukucha wangu. (Walivunja kucha zao.)
- Alikata ukucha kwa kutumia wembe. (Walikata kucha kwa kutumia nyembe.)
- Ukucha wa kati hukua haraka kuliko kucha zingine zote. (Kucha za kati hukua haraka kuliko kucha zingine zote.)