Wingi wa safi ni nini?

Safi ni:

Isiyo na uchafu

Mfano: Hakuwa na nguo safi.

Nadhifu, -limbwende.

-ema.

-siokuwa na dukuduku, -siokuwa na tashwishi.

Mfano: Maelezo safi yalitolewa na mzazi wake.

Visawe vya safi ni: mufti, barabara, sahihi, nadhifu n.k.

Wingi wa safi

Wingi wa safi ni safi.

Neno safi halibadiliki katika wingi, safi katika wingi linapaki kuwa safi.

Mfano katika sentensi

  • Nguo yake ni safi. (Nguo zao ni safi.)
  • Hakuwa na nguo safi. (Hawakuwa na nguo safi.)
  • Maelezo safi yalitolewa na mzazi wake. (Maelezo safi yalitolewa na wazazi wao.)
  • Alitumia lugha safi kueleza. (Walitumia lugha safi kueleza.)
  • Mambo yalimwendea safi alipopata kazi. (Mambo yaliwaendea safi walipopata kazi.)
Related Posts