Kiti ni kifaa kilichotengenezwa kwa mbao, bati, chuma au plastiki kwa madhumuni ya kukalia.
Ukubwa wa neno kiti
Kupata ukubwa wa kiti tunazingatia sheria hii ya ukubwa wa nomino:
Nomino zinazoanza na kiambishi {ki} mwanzoni, kiambishi hicho hudondoshwa katika ukubwa na kiambishi {ji} hupachikwa.
Nomino kiti inaanza na kiambishi {ki} mwanzoni, tunadondosha kiambishi hiki, na kupachika kiambishi {ji}.
Kwa hivyo ukubwa wa kiti itakuwa jiti.
Udogo wa neno kiti
Kupata udogo wa neno kiti tunaongeza kiambishi {ki} kwa ukubwa wa neno kiti.
Udogo wa kiti unakuwa kijiti.
Mfano katika sentensi
Mtu amekalia kiti. [Hali ya kwaida.]
Jitu limekalia jiti. [Hali ya ukubwa.]
Kijitu kimekalia kijiti. [Hali ya udogo.]
Wingi wa udogo na ukubwa wa kiti
Majina ya nomino katika ukubwa huainishwa katika ngeli ya LI-YA. Kupata wingi wa ukubwa tunaongeza kiambishi {ma}.
Majina ya nomino katika udogo huainishwa katika ngeli ya KI-VI. Kupata wingi wa ukubwa tunaongeza kiambishi {vi}.
Kwa mfano
Jitu limekalia jiti. [Hali ya ukubwa.]
Majitu yamekalia majiti. [Hali ya ukubwa wingi.]
Kijitu kimekalia kijiti. [Hali ya udogo umoja.]
Vijitu vimekalia vijiti. [Hali ya udogo wingi.]