Ukubwa wa nomino

Nomino ni jina la mtu, kitu, mahali, tendo au hali.

Nomino zote huwa katika hali ya kawaida. Nomino pia zinaweza kubadilishwa ziwe katika hali ya udogo na ukubwa ili kudhihirisha dhana fulani.

Ukubwa wa nomino

Majina ya nomino katika ukubwa huainishwa katika ngeli ya LI-YA.

Mara nyingi nomino katika ukubwa hujukua viambishi vya umoja {ji/j}. Aidha, viambishi {ma/maji} hutumiwa katika wingi.

Utaratibu wa kuzingatia katika ukubwa wa nomino:

1. Nomino zinazoanza na kiambishi {ki} mwanzoni, na zenye silabi mbili au zaidi, kiambishi hicho hudondoshwa katika ukubwa au kiambishi {ji} hupachikwa.

Mfano:

  • Kibeti = Ukubwa wake ni: beti au jibeti.
  • Kitabu = Ukubwa wake ni:  tabu au jitabu.
  • Kibanda = Ukubwa wake ni: banda au jibanda.
  • Kibanzi = Ukubwa wake ni: banzi au jibanzi.
  • Kibatari = Ukubwa wake ni: batari au jibatari.
  • Kibiriti = Ukubwa wake ni: biriti au jibiriti.
  • Kiboki = Ukubwa wake ni: boko au jiboko.
  • Kidole = Ukubwa wake ni: dole au jidole.
  • Kichane = Ukubwa wake ni: chane au jichane.
  • Kichaka = Ukubwa wake ni: chaka au jichaka.
  • Kifaru = Ukubwa wake ni: faru au jifaru.
  • Kifaraga = Ukubwa wake ni: faraga au jifaranga.
  • Kifuniko = Ukubwa wake ni: funiko au jifuniko.
  • Kifutio = Ukubwa wake ni: futio au jifutio.
  • Kiganja = Ukubwa wake ni: ganja au jiganja.
  • Kigogo = Ukubwa wake ni: gogo au jigogo.
  • Kijiko = Ukubwa wake ni: jiko au jijiko.
  • Kijiti = Ukubwa wake ni: jiti au jijiti.
  • Kikapu = Ukubwa wake ni: kapu au jikapu.
  • Kikombe = Ukubwa wake ni: kombe au jikombe.
  • Kikomo = Ukubwa wake ni: komo au jikomo.
  • Kiluwiluwi = Ukubwa wake ni: luwiluwi au jiluwiluwi.
  • Kinyesi = Ukubwa wake ni: nyesi au jinyesi.
  • King’ora = Ukubwa wake ni: ng’ora au jing’ora.
  • Kitambaa = Ukubwa wake ni: tambaa au jitambaa.
  • Kijani = Ukubwa wake ni: jani au jijani.
  • Kipeopeo = Ukubwa wake ni: peopeo au jipeopeo.

2. Nomino zinazoanza na kiambishi {ki} mwanzoni, kiambishi hicho hudondoshwa katika ukubwa na kiambishi {ji} hupachikwa.

Mfano:

  • Kiatu = jiatu.
  • Kiazi = jiazi.
  • Kibao = jibao.
  • Kichwa = jichwa.
  • Kima = jima.
  • Kinu = jinu.
  • Kinywa = jinywa.
  • Kiti = jiti.
  • Kisu = jisu.

3. Nomino zinazoanza na kiambishi {ch} mwanzoni, kiambishi hicho hudondoshwa katika ukubwa au kiambishi {j} hupachikwa katika wingi.

Mfano:

  • Chuo = juo.
  • Chungu = jungu.
  • Chani = jani.

4. Nomino za ngeli ya LI-YA pamoja na ngeli nyingine zisizokuwa na kiambishi maalum katika umoja, hupachikwa kiambishi {ji} ili kupata ukubwa.

Mfano:

  • Jino = jijino.
  • Kalamu = jikalamu.

5. Herufi {n} inapofuatwa na vokali au nusu irabu, herufi hiyo hudondoshwa kisha herufi {j} hupachikwa.

Mfano:

  • Nyumba = jumba.
  • Nongo = jongo.

6. Nomino zinazoanza na kiambishi {mw} kiambishi hicho hudondoshwa na kupachikwa herufi {j} .

Mfano:

  • Mwalimu = jalimu.
  • Mwembe = jembe.
  • Mwanachama = janachama.
  • Mwanadamu = janadamu.
  • Mwanachuo = janachuo.

7. Nomino zenye sinazoanza na herufi {n} mwanzoni na kufuatwa na konsonanti nyingine kuunda herufi za konsonanti mbili, herufi hiyo hudondoshwa.

Mfano:

  • Nguo = guo.
  • Ndege = dege.

TANBIHI:

Nomino zingine kama vile nzi, nswi, nso n.k. Hupachikwa kiambishi {ji} kuleta ukubwa.

Mfano:

  • Nzi = jinzi.
  • Nswi = jinswi.
  • Nso = jinso.

8. Nomino zenye herufi {m} mwanzoni na zenye silabi moja katika mzizi, herufi hiyo hudondoshwa na kupachikwa kiambishi {ji}.

Mfano:

  • Mtu =jitu.
  • Mke =jike.
  • Mti =jiti.

9. Nomino zilizo na herufi {m} mwanzoni na silabi mbili au zaidi katika mzizi, herufi hiyo hudondoshwa.

Mfano:

  • Mvulana = vulana.
  • Mkono = kono.

10. Nomino zenye herufi {u} mwanzoni na ambazo zina silabi mbili, {j} huongezewa

    Mfano:

    • Uso = juso.
    • Ufa =jufa.

    11. Nomino zenye herufi {u} mwanzoni na zenye silabi zaidi ya mbili, herufi hiyo hudondoshwa.

    Mfano:

    • Ukuti = kuti.
    • Ubongo = bongo.
    • Uyoga = yoga.
    Related Posts