Mti ni mmea mkubwa wenye shina gumu unaoota mwituni au uliopandwa shambani.
Ukubwa wa neno mti
Kupata ukubwa wa mti tunazingatia sheria hii ya ukubwa wa nomino:
Nomino zenye herufi {m} mwanzoni na zenye silabi moja katika mzizi, herufi hiyo hudondoshwa na kupachikwa kiambishi {ji}.
Nomino mti, inaanza na herufi {m} mwanzoni na ina silabi moja ya mzizi, tunadondosha herufi {m} na kupachika kiambishi {ji}. Kwa hivyo ukubwa wa mti ni jiti.
Udogo wa neno mti
Kupata udogo wa neno mti tunaongeza kiambishi {ki} kwa ukubwa wa neno mti.
Udogo wa mti unakuwa kijiti.
Mfano katika sentensi
Mti umevunjika. [Hali ya kawaida,]
Jiti limevunjika. [Hali ya ukubwa.]
Kijiti kimevunjika. [Hali ya udogo.]
Wingi wa udogo na ukubwa wa mti
Majina ya nomino katika ukubwa huainishwa katika ngeli ya LI-YA. Kupata wingi wa ukubwa tunaongeza kiambishi {ma}.
Majina ya nomino katika udogo huainishwa katika ngeli ya KI-VI. Kupata wingi wa ukubwa tunaongeza kiambishi {vi}.
Jiti limevunjika. [Hali ya ukubwa umoja.]
Majiti yamevunjika. {Hali ya ukubwa wingi.]
Kijiti kimevunjika. [Hali ya udogo umoja.]
Vijiti vimevunjika. [Hali ya udogo wingi.]