Udogo na ukubwa wa neno ndovu

Ndovu ni mnyama wa porini aliye mkubwa sana mwenye masikio makubwa na mapana, mkonga ambao huutumia kukata majani ya kula, kuchota maji na pembe mbili ambazo zina thamani kubwa na mara nyingi huwindwa na majangili kwa sababu ya pembe zake.

Ukubwa wa neno ndovu

Kupata ukubwa wa ndovu tunazingatia sheria hii ya ukubwa wa nomino:

Nomino zenye sinazoanza na herufi {n} mwanzoni na kufuatwa na konsonanti nyingine kuunda herufi za konsonanti mbili, herufi hiyo hudondoshwa.

Nomino ndovu inaanza na herufi {n} mwanzoni na kufuatwa na konsonanti nyingine kuunda herufi za konsonanti mbili, kwa hivyo tunadondosha herufi {n} na kupata ukubwa wa ndovu kama dovu.

Udogo wa neno ndovu

Kupata udogo wa neno ndovu tunaongeza kiambishi {ki} kwa ukubwa wa neno ndovu.

Udogo wa ndovu inakuwa kidovu.

Related Posts