Ng’ombe ni mnyama afugwaye lakini mdogo anayefanana na nyati ambaye ana faidea kadhaa kwa mfano nyama, maziwa na ngozi.
Ukubwa wa neno ng’ombe
Kupata ukubwa wa ngombe tunafuata hii sheria ya ukubwa wa nomino:
Nomino zenye herufi {n} mwanzoni na kufuatwa na konsonanti nyingine kuunda herufi za konsonanti mbili, herufi hiyo hudondoshwa.
Neno ng’ombe linaanza na sauti {n} mwanzoni na hufuatwa na konsonanti {g}, kuunda herufi za konsonanti mbili, {ng}. Kwa hivyo, tunadondosha herufi {n} na kupata ukubwa wa ngombe kama gombe.
Udogo wa neno ngombe
Kupata udogo wa neno ngombe tunaongeza kiambishi {ki} kwa ukubwa wa neno ngombe.
Udogo wa ngombe inakuwa kigombe.
Mfano katika sentensi
Ngombe anakula. [Hali ya kawaida.]
Gombe linakula. [Hali ya ukubwa.]
Kigombe kinakula. [Hali ya udogo.]
Wingi wa udogo na ukubwa wa ngombe
Ukubwa wa ngombe, gombe, neno hili linachukua ngeli ya {li -ya}, katika sentensi. Kumaanisha {li} katika umoja na {ya} katika wingi. Na pia unapachika kiambishi {Ma}, kupata wingi wa gombe.
Majina ya nomino katika udogo huainishwa katika ngeli ya KI-VI. Kupata wingi wa ukubwa tunaongeza kiambishi {vi}.
Kwa mfano
Gombe linakula. {Hali ya ukubwa umoja.]
Magombe yanakula. [Hali ya ukubwa wingi.]
Kigombe kinakula. [Hali ya udogo umoja.]
Vigombe vinakula. [Hali ya udogo wingi.]