Mbuzi ni mnyama afugwaye anayefanana na swala.
Ukubwa wa neno mbuzi
Kupata ukubwa wa mbuzi tunafuata sheria hii ya ukubwa wa nomino.
Nomino zilizo na herufi {m} mwanzoni na silabi mbili au zaidi katika mzizi, herufi hiyo hudondoshwa.
Nomino mbuzi huanza na herufi {m} mwanzoni na lina zaidi ya silabi mbili katika mzizi, kwa hivyo tunadondosha herufi {m}.
Kwa hivyo ukubwa wa mbuzi ni buzi.
Udogo wa neno mbuzi
Kupata udogo wa neno mbuzi tunaongeza kiambishi {ki} kwa ukubwa wa neno mbuzi.
Udogo wa mbuzi inakuwa kibuzi.
Mfano katika sentensi
Mbuzi anakula nyasi. [Hali ya kawaida.]
Buzi linakula yasi. [Hali ya ukubwa.]
Kibuzi kinakula kiyasi. [Hali ya udogo.]
Wingi wa udogo na ukubwa wa mbuzi
Majina ya nomino katika ukubwa huainishwa katika ngeli ya LI-YA. Kupata wingi wa ukubwa tunaongeza kiambishi {ma}.
Majina ya nomino katika udogo huainishwa katika ngeli ya KI-VI. Kupata wingi wa ukubwa tunaongeza kiambishi {vi}.
Kwa mfano
Buzi linakula yasi. [Hali ya ukubwa umoja.]
Mabuzi yanakula mayasi. [Hali ya ukubwa wingi.]
Kibuzi kinakula kiyasi. [Hali ya udogo umoja.]
Vibuzi vinakula viyasi. [Hali ya udogo wingi.]