Mji ni penye nyumba nyngi za kuishi watu wengi wenye kufanya shughuli tofauti.
Mfano: Mji mkuu wa nchi, mji ambao ndio makao ya serikali ya nchi.
Mji pia ni nyumba wanamoishi watu wa familia moja.
Mfano: Huu ndio mji wa kaka yangu.
Ukubwa wa neno mji
Kupata ukubwa wa mji tunazingatia sheria hii ya ukubwa wa nomino:
Nomino zenye herufi {m} mwanzoni na zenye silabi moja katika mzizi, herufi hiyo hudondoshwa na kupachikwa kiambishi {ji}.
Nomino mji linaanza na herufi {m} mwanzoni na yenye silabi moja katika mzizi, kwa hivyo tunadondosha herufi {m} na kupachika kiambishi {ji}.
Tukidondosha herufi {m} na kupachika kiambishi {ji}, ukubwa wa mji utakuwa jiji.
Udogo wa neno mji
Kupata udogo wa neno mji tunaongeza kiambishi {ki} kwa ukubwa wa neno mji.
Udogo wa mji inakuwa kijiji.
Mfano katika sentensi
Mji huo ni mzuri. [Hali ya kawaida.]
Jiji hilo ni nzuri. [Hali ya ukubwa.]
Kijiji hicho ni kizuri. [Hali ya udogo.]
Wingi wa udogo na ukubwa wa mji
Majina ya nomino katika ukubwa huainishwa katika ngeli ya LI-YA. Kupata wingi wa ukubwa tunaongeza kiambishi {ma}.
Majina ya nomino katika udogo huainishwa katika ngeli ya KI-VI. Kupata wingi wa ukubwa tunaongeza kiambishi {vi}.
Jiji hilo ni nzuri. [Hali ya ukubwa umoja.]
Majiji hayo ni mazuri. [Hali ya ukubwa wingi.]
Kijiji hicho ni kizuri. [Hali ya udogo umoja.]
Vijiji hivyo ni vizuri. [Hali ya udogo wingi.]