Gari ni chombo cha usafiri chenye magurudumu.
Ukubwa wa neno gari
Mara nyingi nomino katika ukubwa hujukua viambishi vya umoja {ji/j}. Kupata ukubwa wa gari tunafuata sheria hii ya ukubwa wa nomino:
Nomino za ngeli ya LI-YA pamoja na ngeli nyingine zisizokuwa na kiambishi maalum katika umoja, hupachikwa kiambishi {ji} ili kupata ukubwa.
Nomino gari liko katika ngeli ya LI-YA. Kwa hivyo, tunapachika kiambishi {ji} kwa gari ili kupata ukubwa. Ukubwa wa gari utakuwa jigari.
Udogo wa neno gari
Kupata udogo wa neno gari tunaongeza kiambishi {ki} kwa ukubwa wa neno gari.
Udogo wa gari inakuwa kijigari.
Mfano katika sentensi
Gari limesimama kando ya mji. [Hali ya kawaida.]
Jigari limesimama kando la jiji. [Hali ya ukubwa.]
Kijigari kimesimama kando ya kijiji. [Hali ya udogo.]
Wingi wa udogo na ukubwa wa gari
Ukubwa wa gari, jigari, linachukua ngeli ya {li -ya}, katika sentensi. Kumaanisha {li} katika umoja na {ya} katika wingi. Na pia unapachika kiambishi {ma} kupata wingi wa jigari.
Majina ya nomino katika udogo huainishwa katika ngeli ya KI-VI. Kupata wingi wa ukubwa tunaongeza kiambishi {vi}.
Kwa mfano
Jigari limesimama kando la jiji. [Hali ya ukubwa umoja.]
Majigari yamesimama kando ya majiji. [Hali ya ukubwa wingi.]
Kijigari kimesimama kando ya kijiji. [Hali ya udogo umoja.]
Vijigari vimesimama kando ya vijiji. [Hali ya udogo wingi.]