Ndizi ni tunda la mgomba ambalo huweza kukaa idadi kadha pamoja na kufanya shada au kichane na vichane kadha hufanya mkungu.
Mfano: ndizi bokoboko; ndizi kimalindi; ndizi kisukari; ndizi mzuzu; ndizi mshale; ndizi ng’ombe.
Visawe vya ndizi ni: izu, ndovi.
Ukubwa wa neno ndizi
Kupata ukubwa wa neno ndizi tunazingatia sheria hii ya ukubwa wa nomino:
Nomino zenye sinazoanza na herufi {n} mwanzoni na kufuatwa na konsonanti nyingine kuunda herufi za konsonanti mbili, herufi hiyo hudondoshwa.
Neno ndizi huanza na herufi {n} mwanzoni kisha kufuatwa na konsonanti ingine kuunda herufi za konsonanti mbili, kwa hivyo tunadondosha herufi {n} na kupata ukubwa wa neno ndizi kama dizi.
Udogo wa neno ndizi
Kupata udogo wa neno ndizi tunaongeza kiambishi {ki} kwa ukubwa wa neno ndizi.
Udogo wa ndizi inakuwa kidizi.
Mfano katika sentensi
Mtu anakula ndizi. [Hali ya kawaida.]
Jitu linakula dizi. [Hali ya ukubwa.]
Kijitu kinakula kidizi. [Hali ya udogo.]
Wingi wa udogo na ukubwa wa ndizi
Majina ya nomino katika ukubwa huainishwa katika ngeli ya LI-YA. Kupata wingi wa ukubwa tunaongeza kiambishi {ma}.
Majina ya nomino katika udogo huainishwa katika ngeli ya KI-VI. Kupata wingi wa ukubwa tunaongeza kiambishi {ma} na {vi}.
Mfano
Jitu linakula dizi. [Hali ya ukubwa umoja.]
Majitu yanakula madizi. [Hali ya ukubwa wingi.]
Kijitu kinakula kidizi. [Hali ya udogo umoja.]
Vijitu vinakula vidizi. [Hali ya udogo wingi.]