Pika ni kutia nafaka kwa mfano mchele au nyama katika chungu au sufuria na kuiweka kwenye moto hadi iive.
Kinyume cha pika
Kinyume ni neno, tendo kauli au uamuzi unaopinga mambo yalivyokuwa awali au yanavyotarajiwa kuwa.
Kinyume cha neno pika ni pakua.
Pakua ni kutoa chakula kutoka kwenye sufuria au sinia na kukitia katika sahani.
Mfano katika sentensi
Alipika chakula cha wali. – Alipakua chakula cha wali.