Kali ni:
-enye ubapa ulionolewa na unaoweza kukata kitu, -liochongoka.
Mfano: Shoka limenolewa na sasa ni kali.
-enye kupenda kudhuru kwa mfano kuuma, kukaripia na kadhalika.
-enye ladha kama pilipili iwapo mdomoni.
-enye kucheneta mwilini.
Mfano: Jangwani huwa na baridi kali.
Kinyume cha kali
Kinyume cha kali hutegemea ufafanuzi wa hapo juu:
Kinyume cha kali (-enye ubapa ulionolewa) ni butu.
Butu ni:
-siyokuwa na makali.
-siyokata.
Kinyume cha kali (-enye ladha kama pilipili) ni tamu.
Tamu ni -enye ladha ya kupendeza kinywani.
Kinyume cha kali (-enye kupenda kudhuru.) ni rahisi, laini, nyoofu au mpole.
Rahisi ni: sio ghali au sio ngumu.
Laini ni siyo ngumu au siokwaruza.
Kinyume cha kali (-enye kucheneta mwilini) ni nyepesi au tulivu.