Maana ya neno afande na English translation

Maana ya neno afande

Matamshi:  /afandɛ/

afande 1

(Nomino katika ngeli ya [a-wa])

Maana: jina au cheo cha heshima na utiifu kinachotumiwa na askari wa ngazi ya chini wanapomwita mkubwa wao.

afande 2

(Nomino katika ngeli ya [a-wa])

Maana: mwanamume anayetia tupu yake ya mbele katika tupu ya nyuma ya mwanamke au mwanamume. Visawe vyake ni: basha, mfiraji, mlawiti, msenge.

afande! 3

(Kihisishi)

Maana: itiko la heshima linalotamkwa na askari kwa mkubwa wao.

Afande Katika Kiingereza (English translation)

Afande katika Kiingereza  na maana unayokusudia:

Afande (muktadha wa askari) ni: sir.

Afande (msenge) is ni: sodomite.

Related Posts