Maana ya neno aga
Matamshi: /aga/
Aga 1
(Kitenzi)
Maana: punga mkono au sema maneno ya kuashiria kuwa unaondoka.
(Msemo) Aga dunia: kufa, fariki dunia, kata roho.
Mnyambuliko wa neno aga ni: → agia, agika, agisha, agiwa, agwa.
Aga 2
(Kitenzi elekezi)
Maana: funga ukurasa uliokuwa umefunguliwa kwenye tarakilishi. Mnyambuliko wake ni: → agia, agika, agisha, agiwa.
Aga Katika Kiingereza (English translation)
Aga katika Kiingereza inategemea maana unayokusudia:
Aga ya kuashiria kuwa unaondoka ni: to wave goodbye, to bid farewell.
Aga ya funga ukurasa kwa tarakilishi ni: close or exit.