Maana ya neno agua na English translation

Maana ya neno agua

Matamshi: /agua/

(Kitenzi elekezi)

Maana:

1. tibu mgonjwa kwa uganga au dawa za kienyeji. Kisawe ni gangua.

2. bashiri, tabiri, angalilia au fasiri maana ya ndoto. Visawe vyake ni: bashiri, tabiri, piga ramli. Mnyambuliko wake ni: → aguana, agulia, agulika, aguliwa.

Agua Katika Kiingereza (English translation)

Agua katika Kiingereza inategemea maana unayokusudia:

Agua ya kutibu mgonjwa kwa uganga ni: treat with traditional medicine.

Agua ya kubashiri au kutabiri ni: predict, foretell, or interpret dreams.

Related Posts