Maana ya neno ajabu na English translation

Maana ya neno ajabu

Matamshi: /ajabu/

Wingi wa ajabu ni maajabu.

Ajabu 1

(Nomino katika ngeli ya [li-ya])

Maana: jambo au kitu cha kushangaza. Visawe vyake ni: muujiza, kioja, shani.

Ajabu 2

(Kivumishi)

Maana: -iliyopita kiasi. Visawe vyake ni: mno, kupindukia, kiasi.

Mfano: Tatu ni mrembo ajabu.

Ajabu Katika Kiingereza (English translation)

Ajabu katika Kiingereza inategemea maana unayokusudia:

  • Ajabu ya jambo au kitu cha kushangaza ni: a miracle, amazing, astonishing, strange, etc
  • Ajabu ya -iliyopita kiasi ni: Extremely, very, incredibly, really, exceedingly, seriously, super, terrifically, awfully, awful, immensely, and hugely
Related Posts