Maana ya neno ala na English translation

Maana ya neno ala

Matamshi: /ala/

Ala 1

(Nomino katika ngeli ya [i-zi])

Maana: kifuko kinachopachikwa kiunoni cha kuchomekea kisu, jambia au upanga.

Mfano: Ala ya jambia lake imezeeka mno.

Methali: Ala moja haikai panga mbili: Watu wawili wanaogombea kitu kimoja hawawezi kusikilizana.

Ala 2

(Nomino katika ngeli ya [i-zi])

Maana: zana ya kutendea kazi kama vile uundaji wa kitu, uporomoshaji wa muziki.

Ala! 3

(Kihisishi)

Maana: tamko linalofichua hisia za kushangaa au kushtuka.

Ala Katika Kiingereza (English translation)

Ala katika Kiingereza inategemea maana unayokusudia:

  • Ala (kifuko kinachopachikwa kiunoni cha kuchomekea kisu, jambia au upanga) ni: sheath for a knife or dagger.
  • Ala (zana ya kutendea kazi) ni: tool, instrument.
  • Ala! (tamko linalofichua hisia za kushangaa au kushtuka) ni: exclamation of suprise like: Eep! Golly! Ha! Huh! Whoa! Wow! Yikes!
Related Posts