Maana ya neno alasiri
Matamshi: /alasiri/
Alasiri 1
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana: wakati kati ya saa tisa na saa kumi na moja jioni.
Alasiri 2
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana: ibada ya Kiislamu inayofanywa kuanzia saa tisa hadi kabla ya magharibi.
Alasiri Katika Kiingereza (English translation)
Alasiri katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Alasiri (wakati kati ya saa tisa na saa kumi na moja jioni) ni: afternoon.
- Alasiri (ibada ya Kiislamu inayofanywa kuanzia saa tisa hadi kabla ya magharibi) ni: The Muslim afternoon prayer, which is called the Asr prayer.