Maana ya neno alfajiri
Matamshi: /alfajiri/
Alfajiri 1
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana: mapambazuko ya asubuhi sana pale jua linapochomoza mashariki.
Alfajiri 2
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana: ibada ya Waislamu inayosaliwa jua likipambazuka au asubuhi sana.
Alfajiri Katika Kiingereza (English translation)
Alfajiri katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Alfajiri (mapambazuko ya asubuhi ) ni: dawn.
- Alfajiri (ibada ya Waislamu inayosaliwa asubuhi sana) ni: Dawn prayer by Muslims, performed from dawn until sunrise, it is called Fajr prayer.