Maana ya neno amana
Matamshi: /amana/
Amana 1
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana: Kitu anachokabidhiwa mtu ahifadhi hadi mwenyewe anapokihitaji.
Amana 2
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana: kitu kilicho na thamani kubwa.
Amana Katika Kiingereza (English translation)
Amana katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Amana (Kitu anachokabidhiwa mtu ahifadhi hadi mwenyewe anapokihitaji) ni: trust, deposit, security.
- Amana (kitu kilicho na thamani kubwa) ni: a valuable thing.