Maana ya neno amba na English translation

Maana ya neno amba

Matamshi: /amba/

Amba 1

(Kitenzi elekezi)

1. zungumza au sema.

Mfano: Kaka waambaje?

2. sengenya.

Mnyambuliko wake ni: → ambana, ambania, ambanika, ambanisha, ambiwa.

Amba 2

(Kielezi)

Maana: labda, huenda, asaa, pengine.

Amba! 3

(Kihisishi)

Maana: tamko linalotolewa kama kubalio la jambo. Visawe vyake ni: naam, hasa, barabara.

Amba- 4

(Kivumishi)

Maana: kirejeshi cha kutoa sifa za nomino au kiwakilishi chake kifungamanishwacho na “o” rejeshi.

Amba Katika Kiingereza (English translation)

Amba katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:

  • Amba (zungumza au sema) ni: speak.
  • Amba (sengenya) ni: gossip.
  • Amba (tamko linalotolewa kama kubalio la jambo) ni: maybe, perhaps.
  • Amba-(Kivumishi kirejeshi) ni: demonstrative pronoun who.
Related Posts