Maana ya neno ambika
Matamshi: /ambika/
Ambika 1
(Kitenzi elekezi)
Maana:
1. andaa mtego wa samaki kwa nyavu katika maji yenye kina kirefu au maji mafu.
2. tega chambo katika mshipi wa uvuvi.
3. loweka au didimiza majini.
Mnyambuliko wake ni: → ambikia, ambikiana, ambikisha, ambikwa.
Ambika 2
(Kitenzi elekezi )
Maana: zulia au singizia mtu uwongo au habari zisizo kweli.
Mnyambuliko wake ni: Ambikana, ambikia, ambikika, ambikisha, ambikiwa.
Ambika Katika Kiingereza (English translation)
Ambika katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Ambika (andaa mtego wa samaki kwa nyavu katika maji yenye kina kirefu au maji mafu) ni: setting up a fish trap.
- Ambika (tega chambo katika mshipi wa uvuvi) ni: to put a bait on a fishing line.
- Ambika (loweka au didimiza majini) ni: To soak or dip in water, immersing, submerging.
- Ambika (zulia au singizia mtu uwongo au habari zisizo kweli) ni: “slander” or “defamation.” (Making false statements against someone)