Maana ya neno ambilika
Matamshi: /ambilika/
Ambilika 1
(Kivumishi)
Maana: sifa ya mtu unayeweza kumshawishi akubali maoni yako au ya wenzako; mwenye uwezo wa kupokea maoni ya wengine.
Ambilika 2
(Kitenzi si elekezi)
Maana: weza kupokea au kukubali maoni au rai za watu wengine.
Ambilika Katika Kiingereza (English translation)
Ambilika katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Ambilika (sifa ya mtu unayeweza kumshawishi akubali maoni yako au ya wenzako) ni: The quality of someone who can be persuaded to accept your or others’ opinions – open-mindness.
- Ambilika (weza kupokea au kukubali maoni au rai za watu wengine) ni: To be able to receive or accept the opinions or views of others – receptive.