Maana ya neno amili
Matamshi: /amili/
Amili 1
(Kitenzi elekezi)
Maana: jua, fahamu, maizi, tambua, ng’amua, elewa.
Mnyambuliko wake ni: →amilia, amiliana, amilika, amilisha, amiliwa.
Amili 2
(Kitenzi elekezi)
1. tenda kazi au shughuli. Kisawe chake ni shughulika.
2. unda au tengeneza.
3. karabati au rekebisha kitu kilichoharibika.
Mnyambuliko wake ni: → amilia, amiliana, amilika, amilisha, amiliwa.
Amili Katika Kiingereza (English translation)
Amili katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Amili (jua, fahamu, maizi, tambua, ng’amua, elewa) ni: know, realize, decide, understand.
- Amili (tenda kazi au shughuli) ni: work.
- Amili (unda au tengeneza) ni: create.
- Amili (karabati au rekebisha kitu kilichoharibika) ni: repair.