Maana ya neno amka
Matamshi: /amka/
(Kitenzi si elekezi)
Maana:
1. toka kitandani au usingizini; fumbua macho.
Mfano: Babake Juma amechelewa kwenda uvuvini kwa sababu hakuamka alfajiri.
2. janjaruka, zinduka, changamka au erevuka.
3. simama wima au inuka.
Mfano: Mgeni wa heshima alipoingia ukumbini, watu wote waliaka na kusimama.
Mnyambuliko wake ni: → amkia, amkika, amkisha, amkiwa.
Amka Katika Kiingereza (English translation)
Amka katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Amka (toka kitandani au usingizini; fumbua macho) ni: wake up, arise.
- Amka (janjaruka, zinduka, changamka au erevuka) ni: become active, wise.
- Amka (simama wima au inuka) ni: stand up, arise.