Maana ya neno amkia
Matamshi: /amkia/
Amkia 1
(Kitenzi elekezi)
Maana: amkua, sabahi, salimu mtu; julia mtu hali.
Mfano: Juma huwaamkia wazazi wake kila asubuhi.
Mnyambuliko wake ni: → amkiana, amkika, amkilia, amkisha, amkiwa.
Amkia 2
(Kitenzi si elekezi)
Maana: mkesha wa; tangulia siku fulani.
Mfano: Mwezi umeandama kwa hiyo kesho tutaamkia Sikuu ya Idd.
Amkia Katika Kiingereza (English translation)
Amkia katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Amkia (amkua, sabahi, salimu mtu; julia mtu hali) ni: greet, accost, salute.
- Amkia (mkesha wa; tangulia siku fulani) ni: the eve of; a day that precedes a certain day.