Kunguni ni wadudu wa rangi ya rangi nyekundu ama kahawia wasio na mabawa ambao hula tu damu ya wanyama na binadamu. Uvamizi wa kunguni umeongezeka sana katika miaka michache iliyopita. Katika makala haya tutaona mahali kunguni wanapenda kuishi, kunguni husababishwa na nini, dalili za kunguni na jinsi ya kuzuia kunguni.
Kunguni husababishwa na nini?
Kunguni wanaweza kuhama kutoka mahali moja hadi nyingine kwa kusafiri kwa vitu kama vile nguo, mizigo, masanduku, matandiko n.k.
Kunguni wanaweza kusafiri kwa urahisi kati ya sakafu na vyumba vinavyokaribiana.
Unaweza pia kupata kunguni kutoka kwa:
- hoteli, hosteli
- mabweni
- usafiri wa umma, kama vile mabasi, treni, teksi na magari ya umma
Kunguni hawajali kama nyumba yako ni safi au chafu. Wanachohitaji ni mahali pa joto na sehemu nyingi za kujificha.
Kunguni wanaishi wapi?
Wanaweza kubarizi katika kila aina ya vitu kama:
- magodoro
- shuka na blanketi
- maeneo karibu na kitanda chako
- maeneo ya vitu vingi ambavyo havisogezwi mara kwa mara, kama vile milundo ya nguo
- chini ya ukuta
- chini ya mazulia kwenye kingo za nje, kama vile karibu na mbao
- nguo
- masanduku au vitu vingine vya mizigo
Baadhi ya dalili za kunguni
Je, huna uhakika kama una kunguni au kitu kingine? Hizi hapa ni dalili za kunguni:
- Ngozi inawasha mahali uliumwa. Kuumwa na kunguni ni vipele vidogo vinavyowasha vinavyofanana na kuumwa na mbu.
- Makundi ya uvimbe mahali ulimwa. Hizi kawaida hukusanyika katika eneo ndogo la ngozi yako mahali kunguni alikuuma.
- Madoa madogo ya damu kwenye blanketi zako. Hii inaonyesha mahali ambapo ngozi iliyoumwa imegusana na matandiko yako.
- Njia za kunguni ni madoa madogo meusi au kupaka kwenye vitanda.
Jinsi ya kuzuia kunguni
- Funika mwili wako na nguo unapolala. Kunguni hawaumwi kama umevaa nguo.
- Kagua mitumba. Angalia matandiko yaliyotumika na vitu vingine vya mitumba, kwani vinaweza kuwa na kunguni.
- Tumia tahadhari ukiwa kwa mahali watu wengi hukuwa kama kwa magari ya umma na hoteli.
- Safisha na uondoe uchafu, hasa katika chumba chako cha kulala.
- Sogeza kitanda chako mbali na kuta.
- Safisha madirisha na sakafu kila siku.
- Osha shuka, mito, blanketi na na matandiko ya kitanda na uviweke kwa jua.
- Ziba nyufa na uwazi wowote ambapo wanaweza kuingia kwa nyumbani.
One response to “Kunguni husababishwa na nini? Na jinsi ya kuzuia”