ubuyu

Ubuyu in English – Faida za kiafya za ubuyu

Posted by:

|

On:

|

,

Ubuyu ni nini?

Ubuyu ni ungaunga wa matunda ya mbuyu.

Ubuyu in English

Baobab nut/seed: Hii ndiyo tafsiri halisi ya “ubuyu” in English. Ufafanuzi wake kwa Kiingereza ni:

“Edible seeds or pith of the baobab tree, which can be cooked and eaten in various ways.”

Faida za kiafya za ubuyu

  • Iko na virutubisho kadhaa
  • Husaidia kupunguza uzito
  • Hudhibiti sukari ya damu
  • Hupunguza Kuvimba
  • Husaidia usagaji wa chakula
  • Lishe bora

Iko na virutubisho kadhaa

Ubuyu umejaa vitamini na madini muhimu kama vitamini C, antioxidants, potasiamu, magnesiamu, chuma, zinki, kalsiamu, na vitamini B. Iwe katika hali yoyote; unga,mbegu au mbichi, iko na aina hizi mbalimbali za virutubisho.

Husaidia kupunguza uzito

Kuongeza ubuyu kwenye lishe yako kunaweza kusaidia kupunguza uzito kwa kuzuia hamu ya kula kwani unakufanya huhisi kama umeshiba kwa muda. Iko na fiber nyingi ambazo hupunguza usagaji wa chakula, na hivyo kupunguza ulaji wa jumla wa kalori na uzito wa mwili.

Hudhibiti sukari ya damu

Mbuyu unaweza kusaidia kudhibiti viwango vya sukari kwenye damu. Uchunguzi unaonyesha kuwa inapunguza wanga iliyo kwa mkate, na hivyo kupunguza kasi ya kuongezeka kwa sukari ya damu.

Hupunguza kuvimba

Ubuyu hulinda seli kutokana na uharibifu wa maambukizi na inaweza kupunguza kuvimba. Hii ni kutokana na utafiti uliofanywa kwa wanyama, utafiti zaidi kwa wanadamu unahitajika kufanyika kuelewa athari zake kikamilifu.

Husaidia usagaji wa chakula

Kiwango cha juu cha fiber katika ubuyu huchangia afya ya usagaji chakula. Huongeza mzunguko wa kinyesi na inaweza kulinda dhidi ya hali kama vile kuvimbiwa na ugonjwa wa matumbo.

Lishe bora

Iwe imeliwa mbichi, mbegu au katika hali ya unga, mbuyu ni lishe bora na unaweza kuiongeza kwa kwa mapishi mbalimbali.