Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume

Nguvu za kiume

Tatizo la nguvu za kiume ni hali ya mwanaume kushindwa kusimamisha uume au kudumisha usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la ndoa.

Makala haya yanaangazia njia za asili za kutibu tatizo la nguvu za kiume. Njia hizi zimethibitishwa kuwa na ufanisi katika kutibu tatizo hili, na ni salama kutumia.

Tatizo hili linaweza kusababishwa na mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:

Sababu za upungufu wa nguvu za kiume:

  • Umri
  • Magonjwa kama kisukari, shinikizo la juu la damu, na uzito kupita kiasi
  • Matumizi ya vilevi kama pombe na sigara
  • Ukosefu wa mazoezi ya viungo
  • Msongo wa mawazo
  • Uvutaji sigara
  • Utumiaji uliozidi wa kafeina
  • Kudhurika kwa neva au uti wa mgongo
  • Madawa ya kulevya
  • Kupunguka kwa homoni ya testerone
  • Athari kutoka kwa baadhi ya dawa
  • Unywaji Pombe uliokithiri

Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume

  • Acha mawazo
  • Jitibu magonjwa yanayosababisha tatizo
  • Acha vilevi
  • Fanya mazoezi ya viungo
  • Tumia kitunguu swaumu
  • Kula tikiti maji
  • Kula ugali wa dona
  • Tumia chumvi ya mawe
  • Kunywa maji mengi kila siku
  • Tafuna mbegu za maboga
  • Kula asali mbichi
  • Kula korosho
  • Kula mdalasini
  • Kula tangawizi
  • Kula ndizi
  • Kula matunda na mboga

Kitunguu saumu

Kitunguu swaumu ni dawa ya asili ambayo ina uwezo wa kutanua mishipa ya damu, na hivyo kuongeza mtiririko wa damu kwenda kwenye uume.

Tikiti maji

Tikiti maji lina virutubisho muhimu kama vile Calcium, Magnesium, Carotene na vitamin lukuki ikiwemo A, B6 na C ambavyo kwa pamoja hutengeneza virutubisho muhimu vya kuboresha nguvu za kiume.

Ugali wa dona

Ugali wa dona ni chanzo kizuri cha madini ya zinki, ambayo ni muhimu kwa utendaji kazi wa kawaida wa tezi dume.

Chumvi ya mawe

Chumvi ya mawe ina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume kwa kusaidia mwili kunyonya virutubisho muhimu.

Maji mengi

Maji ni muhimu kwa afya ya jumla, ikiwa ni pamoja na afya ya uume. Kunywa maji mengi husaidia kuondoa sumu mwilini na kuboresha mtiririko wa damu.

Mbegu za maboga

Mbegu za maboga ni chanzo kizuri cha virutubisho ambavyo vinasaidia kuongeza nguvu za kiume, ikiwa ni pamoja na vitamini E, magnesiamu, na zinc.

Parachichi

Parachichi ina vitamin E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni zinazochochea kuongezeka kwa uimara wa nguvu za kiume na kuleta msisimko wa hali ya juu wakati wa kushiriki tendo la ndoa.

Banana shake

Ndizi mbivu ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia kuongeza stamina na nguvu mwilini, hasa wakati wa kufanya kazi nzito.

Ndizi pia ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume na ashki ya mapenzi (Libido).

Maziwa

Maziwa ya fresh au mtindi yanaongeza nishati na nguvu ya kushiriki tendo la ndoa bila kuchoka.

Juisi ya komamanga

Komamanga ina kiwango kikubwa cha antioxidants ambayo husaidia kuongeza kasi ya mzunguko wa damu na kuzuia magonjwa ya moyo. Mzunguko wa damu wenye afya husambaza damu ya kutosha katika viungo vyote vya mwili ikijumuisha pia damu iliyo katika mishipa ya uume.

Juisi ya tikitimaji

  • Tengeneza juisi ya tikiti maji na tangawizi kwa kutumia maziwa fresh.
  • Chuja juisi hiyo na mimina vijiko kadhaa vya asali.
  • Kunywa mara moja tu kwa siku au japo kwa wiki mara nne hadi tano.

Ni moja ya booster na tiba nzuri sana kwa wanaume ambao uwezo wao kitandani unaonekana kuanza kupungua.

Kama umeathiriwa sana na michezo ya punyeto au changamoto za muda mrefu za kukosa nguvu za kiume:

  • Tafuta tangawizi kubwa nne au sita, vitunguu saumu ujazo wa glass moja, unga wa msamitu vijiko nane, unga wa mdalasini vijiko sita mpaka nane, unga wa habat sawda (black seed) vijiko vinne mpaka sita.
  • Saga tangawizi na vitunguu saumu kwenye blenda.
  • Weka unga wa msamitu, mdalasini na unga wa habat sawda kwenye blenda kisha ukiwa umewasha blenda mimina taratibu asali mbichi lita nzima iishe, kwa muda wa kama dakika mbili juisi yako itakuwa tayari.
  • Baada ya masaa sita, juice yako itakuwa tayari kwa matumizi

Matumizi:

Utakuwa ukilamba vijiko viwili asubuhi unapoamka kabla hujala chochote, na usiku utatumia tena vijiko vitatu kabla ya kulala.

Njia za kuzuia tatizo la nguvu za kiume

  • Kuepuka mambo yanayoweza kusababisha tatizo hili, kama vile matumizi ya vilevi, punyeto, uvutaji sigara, na ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi.
  • Kuishi maisha yenye afya, ikiwa ni pamoja na kula mlo kamili, kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara, na kupumzika vya kutosha.
Related Posts