,

Biashara ya muda mchache

Katika makala haya, nitachunguza fursa za biashara zenye hazichukui muda mwingi na ambazo zinahitaji uwekezaji mdogo na zinazotoa uwezekano mkubwa wa faida.

Biashara inayochukua muda mfupi

Kufundisha.

Watoto wakiwa nyumbani, na ukiwa na ujuzi wa kufunza, uliza wazazi wao wakulipe ili uwafunze. Unaweza kufundisha masomo mbalimbali yanayofundishwa shuleni.

Kuuza chakula kilichopikwa kwa wanafunzi

Ikiwa unafurahia kupika, zingatia kupata mapato ya ziada kwa kuuza chakula kilichopikwa nyumbani kwa wanafunzi wenye njaa karibu na taasisi za elimu.

Inahitaji uwekezaji mdogo katika vifaa vya msingi vya kupikia na viungo, unaweza kupika chakula mbalimbali ambazo wanafunzi hupenda, kama vile githeri, chapati na mandazi.

Uuzaji wa viatu.

Uza viatu vipya kabisa au vya mitumba vya watoto, wanaume na wanawake. Unahitaji pesa ndogo kuanzisha hii.

Biashara ya chipsi

Kuanzisha biashara ya chipsi inahitaji gharama ndogo na ina faida inayovutia. Utahitaji viungo muhimu kama viazi, mafuta ya kupikia, na kuni ama makaa, pia unaenza tumia stima.

Mahali ya biashara ni muhimu, kwa hivyo zingatia kuweka karibu na shule, au mitaa yenye shughuli nyingi ambapo watu hukusanyika.

Pata pesa mtandaoni.

Chukua wazo lako mtandaoni na uligeuze kuwa biashara yenye faida. Tangaza bidhaa na huduma zako kwenye mtandao. Pata wateja na uendelee kukuza biashara yako.

Kuchoma Mahindi

Mahindi ya kuchoma ni chakula maarufu cha mitaani barani Afrika na kinaweza kuwa biashara yenye faida. Gharama ya kuanza ni ndogo, inahitaji mahindi safi na makaa ya kuchoma.

Kupata eneo lenye shughuli nyingi, haswa wakati wa kilele, ni muhimu. Kuweka kibanda chako karibu na shule, soko, vituo vya mabasi, au mitaa yenye shughuli nyingi kunaweza kuvutia wapita njia wenye njaa.

Kibanda

Kuanzisha duka dogo la mboga katika mitaa yenye shughuli nyingi kunaweza kuwa mradi mzuri. Zingatia kuuza vitu muhimu vya kila siku kama mboga, matunda, nafaka na vitu vya nyumbani. Mahali ni muhimu, kwa hivyo chagua eneo la kimkakati karibu na maeneo ya makazi au soko.

Kilimo cha mboga.

Panda na uuze vitunguu, cabbage, sukuma au mboga nyingine. Unaweza pia kupata mboga kutoka kwa wakulima wengine na kufanya biashara yako ya kununua na kuuza kwa faida.

Boda boda.

Toa huduma za kuaminika ukitumia pikipiki yako. Nunua pikipiki na uingie kwenye biashara ya usafirishaji. Wasaidie majirani zako wafike kazini au nyumbani.

Mitungi ya gesi.

Ingia katika biashara ya kuuza mitungi ya gesi, kwa kutoa huduma za kujaza na kuuza gesi na vifaa vya gesi.

Kuuza sabuni ya kutengenezewa nyumbani

Jifunze kutengeneza sabuni na uuze. Unahitaji viungo visivyo na gharama na vifaa vya kufungaj ili kuanza. Tangaza sabuni zako ulizotengeneza kwa mtandaoni au katika masoko ya kwenu ili kufikia watu wengi.

Fotokopi.

Ingia katika biashara hii na utazame biashara yako ikikua kila wakati mpiga fotokopi anapotoa ukurasa umpigie fotokopi. Huduma nyingine unaweza kutoa kwa kushirikiana na hii: ni lamination na huduma za mtandaoni.

Duka la sinema.

Uuza filamu. wasaidie watu wapate filamu na vipindi vyao vya televisheni wavipendavyo – Hollywood, Nollywood, Bollywood na sehemu nyinginezo za dunia.

Kilimo cha kisasa.

Fuga kuku, sungura au ng’ombe wa maziwa na uuze mazao kwa majirani au makampuni mbalimbali. Unaweza pia sambaza kwa shule za jiji.

Anzisha kiwanda kidogo cha kuoka mikate

Uwekezaji katika viungo vya msingi vya kuoka kama vile unga, sukari, mayai na chachu inatosha kuanza.

Lenga wanafunzi au maduka makubwa ya karibu kama msingi wa wateja wako. Oka na kuuza keki kwa hafla tofauti. Unaweza kupika keki za harusi, keki za siku ya kuzaliwa – au keki kwa hafla mbalimbali kama vile Siku ya wapendanao, siku ya akina mama na siku ya akina baba.

Kuosha gari na pikipiki.

Ikiwa unapenda kuondoa uchafu na kulipwa kwa nini usianzishe biashara ya kuonsha gari na pikipiki?

Kinyozi.

Ingia katika biashara ya kusaidia watu kutengeneza nywele jinsi wanavyotaka, hii inahitaji kipanda kilicho na stima na mashine ya kunyoa.

Upigaji picha

Hii ni biashara yenye gharama ya chini kiasi ya kuanza na ukiwa na zana zinazofaa, unaweza kuianzisha ukiwa nyumbani kwako. Upigaji picha wa kitaalamu unahitajika sana kwa matukio mbalimbali kama vile harusi, mikusanyiko ya kijamii, picha za familia, miongoni mwa mengine.

Saluni ya kuenda kwa wateja

Iwapo una ujuzi wa kutengeneza nywele, kutengeneza kucha, fikiria kuanzisha biashara ya saluni ya kuenda nyumba kwa nyumba. Mbinu hii bunifu inahusisha kupeleka huduma zako za saluni moja kwa moja kwenye milango ya wateja, kuwapa urahisi na ubora.

Related Posts