Mbinu Ya Kupata Pesa Online($ 300 Kwa Mwezi) Kutoka Kwa Clickworker.

Posted by:

|

On:

|

Clickworker hutoa kazi kwa wafanyikazi waliosajiliwa kwa mtandao. Kama ilivyo kwa mashirika mengine, Clickworkers wanatakiwa kujiandikisha kabla ya kuanza kazi yake. Katika chapisho hili, nitakuonyesha jinsi ninavyopata mapato ya muda kutoka kwa Clickworker. Pesa hiyo inatosha kulipa gharama za chakula na kodi.

Clickworker

Clickworker inatoa fursa nzuri ya kupata pesa pamoja na ajira yako au kujiajiri. Tafadhali kumbuka kuwa huwezi kupata riziki ya muda mrefu kutoka kwa Clickworker, lakini unaweza kupata pesa nzuri za kukidhi mahitaji yako. Kwa mfano hizi ndizo pesa nilitengeneza kwa muda wa miezi sita nilizo fanya kazi kwa Clickworker, kupitia kufanya kazi kwa mshirika wake UHRS. (Ambapo grafu ya mstari iko chini sana, inamaanisha kuwa miezi hiyo sikufanya kazi, kama vile kutoka Novemba 2022 hadi Juni 2023.)

Nilitengeneza jumla ya Us Dollars $1,550. Ukigeuza ikuwe pesa ya Kenya itakuwa Ksh. 217,000 (1550*140). Na kwa pesa ya Tanzania itakuwa Tzs. 3,844,00 (1550*2480). Kwa miezi sita hii ni pesa nzuri, sivyo?

Jinsi ya kupata mapato kupitia Clickworker

Hebu tuanze jinsi ya kupata mapato kupitia Clickworker (hata kama unatumia simu). Kumbuka kwa makini kwamba kufuata hatua hizi nitakazotoa, kutakuhakikishia kuwa utakubaliwa kwa Clickworker na kupata ufikiaji wa kazi zinazolipa zaidi. Kwa hivyo tafadhali fuata links zote nitakazokupea na utaongeza nafasi zako za kutengeneza pesa.

Kujisajili

Unaweza kujisajili na Clickworker kwa kwenda kwenye tovuti hii clickworker.com. Mara baada ya kubofya link hii, pata link ya kujiandikisha na ubofye juu yake. Utaelekezwa kwenye ukurasa mwingine wa kujisajili. Hakikisha umefuata hii link, na umebofya “register” harafu “For clickwoker” ndio ukubaliwe.

Jaza form

Kutoka hapo, utahitajika kujaza maelezo yako ya msingi. Hii ni pamoja na jina lako, barua pepe, anwani na mambo mengine machache.

Baada ya kujiandikisha kwa mafanikio, utapata kazi rahisi ambazo unaweza kufanya. Lakini kazi hizi hazitakupa pesa zaidi. Kwa hivyo tutaenda hatua inayofuata.

Jaza taarifa zaidi

Sehemu hii ni muhimu sana. Utawasilishwa na form ili kujaza maelezo yako. Hakikisha umeyajaza maelezo yote kwa usahihi iwezekanavyo, hasa uwezo wako wa lugha. Kwani ukijaza maelezo yako itakuwa vingumu sana kubadilisha baadaye.

Chagua lugha unayoifahamu vizuri, inaweza kuwa Kijerumani, Kifaransa, Kihispania n.k. Lugha kama Kijerumani na Kifaransa zina kazi zinazolipa pesa nyingi sana, kwa hivyo ikiwa unajua lugha hizi, unaweza kupata riziki nzuri kutoka kwa tovuti hii.)  (hakikisha umejaza kuwa wewe ni mzungumzaji asili wa Kiingereza (native speaker) ama lugha utakayoichangua)

Fanya tathmini (Complete Assessments)

Ukishajaza maelezo yako, utaelekezwa kwingine kuchukua tathmini ili kupima uwezo wako wa Kiingereza ama lugha ya msingi uliyoichangua. Fuata maagizo yote na ukamilishe tathmini. Fanya bidii sana upate juu ya asilimia 75. Lakini usiwe na wasiwasi kwa sababu maswahili si ngumu.

Kamilisha tathmini nyingine mbili (UHRS Assessments)

Kutakuwa na tathmini mbili zaidi ambazo utahitaji kukamilisha: UHRS I na UHRS II. Majaribio haya yanaweza tu kufikiwa pindi tu unapokamilisha taarifa zote (under profile) (hakikisha umejaza kuwa wewe ni mzungumzaji asili wa Kiingereza ama lugha utakayoichangua).

Hizi assessments ni rahisi kama ulipita ya kwanza. UHRS I ni kama tathmini ya hapo awali na UHRS II  inakuhitaji uunde akaunti ya barua pepe ukitumia Outlook ama Hotmail, inayoitwa “Live Id”. Baada ya kukamilisha kuunda “Live Id”. Hakikisha umeiandika chini na nenosiri (password). Hili ni jambo ambalo hutaki kusahau.

Ongoja muda mchache Clickworker waactivate akaunti yako. After wameactivate utakuwa huru kuingia kwa UHRS na kupata kazi za kufanya.

(Pia kumbuka utahitajika kufungua akaunti ya PayPal, ambapo pesa zitaingia). Baada ya kujisajili pia utalazimika kudownload Clickworker App kutoka kwa Google Playstore.

Pia utapewe link ya kudownload UHRS app ya simu, mahali utafanyia kazi yako na simu.

Mara tu unapoingia, utawasilishwa na orodha ya kile kinachoitwa “HitApps.” HitApps hizi ni njia nyingine ya kusema kazi ambazo unapaswa kufanya.

Kabla ya kuweza kufanya kazi, itabidi upitie awamu ya kufuzu. Mara tu utakapomaliza kufuzu, hutalazimika kufuzu tena.

Utapokea idadi chache tu ya nafasi za kufuzu kwa hivyo hakikisha kuwa mwangalifu. Ukishindwa kufuzu, hutaweza kufanya kazi hiyo tena. Ukifuata sheria za “HitApp” itakuwa rahisi sana kwako kupita.

Ili kufanikiwa katika UHRS na kupata pesa nyingi, chagua kazi zinazolipa pesa nyingi na zinazochukua muda kidogo kukamilisha.

Je, utalipwa lini?

Unapojisajili kwa mara ya kwanza na kukamilisha kazi UHRS itachukua siku 39 ndio upate malipo yako ya kwanza. Baada ya hapo, unalipwa kila wiki. Pesa kutoka UHRS yako zitaonekana katika akaunti yako ya Clickworker kila Jumatatu hivi. Kutoka hapo kila Alhamisi pesa huwekwa kiotomatiki kwenye akaunti yako ya PayPal.

Fuata hii link kujisajili: